http://samchardtz.blogspot.com/2014/05/kituko-cha-mwaka-wazazi-waisusa-maiti.html

Kijana Leonard Jorome Mwakanyamale,enzi za uhai wake
Tofauti
na desturi ya Kitanzania watu kuwa pamoja katika kipindi cha matatizo,
wazazi wa marehemu, Leonard Jorome Mwakanyamale, wanadaiwa kususa kuzika
maiti ya mtoto wao kisa ugomvi kati ya marehemu na nduguze.
Leonard ambaye
alikuwa akiishi Buguruni jijini Dar, alifariki dunia Mei 10, mwaka huu
kwa Ugonjwa wa Malaria.Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa jirani mmoja
ambaye hakutaka jina lichorwe gazetini, Leonard alikuwa na ugomvi na
familia yake na aliapa kutokanyaga kwao mkoani Mbeya tangu alipokwenda
kumzika bibi yake, zaidi ya miaka mitano iliyopita.“Tangu nijuane na
Leonard zaidi ya mwaka wa tano, hajakanyaga kwao.
“Nilisikia mara ya mwisho kwenda kwao ilikuwa msiba wa bibi yake.“Tunasikia
wakati anatoka Mbeya kuna maneno yaliwakera wazazi wake, inawezekana
ndiyo yamewachefua na kushindwa kumsamehe kwani nasikia alidai hatarudi
tena Mbeya kwa kuwa watu aliokuwa akiwapenda walishamalizika, yaani bibi
yake.

Mwili wa Leonard Jorome Mwakanyamale,ukiwa makabulini tayali kwa mazishi
“Sijui
kwa nini alisema maneno hayo japokuwa uwezo wa kumsafirisha ulikuwepo
kabisa lakini wazazi walikataa asipelekwe kwa kuwa alipasusa kwao hivyo
azikwe Dar es Salaam na siyo mkoani Mbeya,” alisema jirani huyo.Jitihada
za kuwatafuta ndugu wa marehemu ziligonga mwamba kwani simu zao
hazikuwa hewani, kupitia habari hii wakiisoma, wanaweza kutoa ufafanuzi.Naye
mke wa marehemu, Letisia Mbilite hakuwa tayari kuzungumzia suala hilo
kwani alikuwa haamini kilichotokea na alikuwa na majonzi mazito.Baada
ya wazazi kutokubali kushiriki mazishi ya mtoto wao, marafiki
waliungana, wakauhifadhi mwili katika Hospitali ya Amana, Dar kisha
kusomewa misa na Mwenyekiti wa Kanisa la Parokia ya Stephano, Shahidi
Anton Makala na kuzikwa katika Makaburi ya Wailes yaliyopo Chang’ombe,
Dar