KINANA KATIKA KATA YA KITUNDA
http://samchardtz.blogspot.com/2014/05/kinana-katika-kata-ya-kitunda.html
Katibu
Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa kijiji cha Mgambo
katika kitongoji cha Lukula kata ya Kitunda wilayani Sikonge mkani
Tabora ambapo aliwaomba radhi wakulima wa Tumbaku kwa kadhia waliyo nayo
kutokana na kunyonywa na kutopata haki zao za malipo kwa miaka 3.
Katibu
Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana pamoja na Mbunge wa Jimbo la Sikonge
Said Mkumba wakiwasomea wananchi wa kijiji cha Lukula maeneo
yatakayopata umeme mwaka huu katika wilaya ya Sikonge.
Mbunge wa
Jimbo la Sikonge, Said Mkumba akihutubia wananchi wa kijiji cha Lukula
kata ya Mgambo na kuwaambia wale wote waliodhulumu wakulima wanatakiwa
kuchukuliwa hatua na pia alisisitiza sheria zingatiwe za wanasiasa
kutojihusisha na masuala ya vyama vya ushirika.
Katibu
Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akipata maelezo ya ujenzi wa jengo la
upasuaji kwa Dk.Silvanus Kabutura ambaye pia ni Mganga Mfawidhi wa kituo
cha afya cha Kata ya Kitunda wilayani Sikonge, Daktari Kabutura
alimueleza Katibu Mkuu wa CCM changamoto kubwa uhaba wa maji katika
kituo hicho.
Katibu
Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akitoka kukagua jengo la upasuaji la
kituo cha afya cha Kitunda wilayani Sikonge, mkoani Tabora ambalo
limechelewa kukamilika kwa zaidi ya mwaka mmoja na huku Wizara ya Afya
kushindwa kuchukua hatua mpaka sasa.