HUU NI UJUMBE WA MENEJA WA TWANGA BW. HASSAN REHAN KUHUSU MAANDALIZI YA ABLUM YAO MPYA
http://samchardtz.blogspot.com/2014/05/huu-ni-ujumbe-wa-meneja-wa-twanga-bw.html
Twanga kutoka na moja mmpya BE NDI ya muziki wa dansi ya African Stars International ‘Twanga Pepeta’ imeanza kutayarisha nyimbo ambazo zitakuwemo kwenye albamu yao mpya. Akizungumza na mtandao huu, meneja wa bendi hiyo Hassan Rehani, alisema kuwa wana vyimbo nyingi, lakini kwa sasa wamekamilisha wimbo mmoja, ambao wanafanya mpango kwa ajili ya kuingia studio na kurekodi. “Tumeanza kutayarisha nyimbo mpya kwa ajili ya albamu ijayo, hivyo tunaendelea kuzifanyia mazoezi kabla ya kuingia studio kwa ajili ya kuzirekodi na kwa sasa wimbo ambao uko kamili ni mmoja,” alisema Hassan. Wimbo huo ambao uko tayari unaitwa Mapenzi Yanauma,(JONATHAN TITO)


