CCM ‘kuishambulia’ Ukawa kwa siku 26
http://samchardtz.blogspot.com/2014/05/ccm-kuishambulia-ukawa-kwa-siku-26.html

Kwa ufupi
Wakati
Kinana akifanya ziara katika mikoa hiyo, Mwenyekiti wa Umoja wa Wazazi
wa CCM, Abdallah Bulembo amekwishaanza kushambulia Mikoa ya Kusini,
Lindi, Mtwara, Ruvuma, Njombe na Iringa.
Dar es Salaam.
Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), wanaanza ziara ya siku 26 katika
Mikoa mitatu ya Tabora, Singida na Manyara kukagua uhai wa chama na
maandalizi ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa baadaye mwaka huu.
Hata
hivyo, duru za kisiasa zinaonyesha kuwa ziara hiyo ni sehemu ya
kuushambulia Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), ambao walitoka bungeni
wakati wakijadili mchakato wa Katiba Mpya wakidai kutoridhishwa na
mwenendo wa Bunge hilo. Ukawa pamoja na CCM walikwishafanya hivyo
Zanzibar.
Wakati
Kinana akifanya ziara katika mikoa hiyo, Mwenyekiti wa Umoja wa Wazazi
wa CCM, Abdallah Bulembo amekwishaanza kushambulia Mikoa ya Kusini,
Lindi, Mtwara, Ruvuma, Njombe na Iringa.
Katibu wa
Halmashauri Kuu ya CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nauye alisema Katibu
Mkuu wa chama hicho, Abdulrahman Kinana ataanza ziara yake Mkoa wa
Tabora, ambako atatembelea wilaya zote kuanzia Mei 8 hadi 18. Mkutano wa
kwanza utaanza leo katika Wilaya ya Igunga.
Baadaye
ataendelea Mkoa wa Singida kuanzia Mei 19 hadi 26 na kumalizia Mkoa wa
Manyara, ambako ataanza Mei 26 hadi Juni 3 mwaka huu.
Nape
alisema pia kuwa wamemkabidhi Waziri Mkuu, Mizengo Pinda ripoti ya
utekelezaji wa ilani ya uchaguzi katika Mikoa ya Kigoma, Rukwa na Katavi
ili afahamu changamoto za mikoa hiyo.
Nape
alisema kuwa ripoti hiyo inahusu changamoto na mafanikio ambayo
yamebainika katika ziara ya Katibu Mkuu wa CCM, Kinana aliyoifanya hivi
karibuni katika mikoa hiyo. CHANZO:MWANANCHI