BENKI YA CRDB YATOA MSAADA SHULE YA SEKONDARI YA WASICHANA KIBOSHO
http://samchardtz.blogspot.com/2014/05/benki-ya-crdb-yatoa-msaada-shule-ya.html

Mkurugenzi
Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akisaini kitabu cha wageni
alipofika katika Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Kibosho, wakati wa
mahafali ya Kidato cha Sita. Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Shule, Mhandisi Aloyce Peter Mushi.
Mkuu
wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Kibosho, Sista Anna akimpeana
mkono na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei wakati
wa mahafali ya Kidato cha sita yaliyofanyika Shuleni hapo. Benki ya CRDB
ilitoa msaada wa shs. milioni 5 na katika harambee iliyofanyika shuleni
hapo jumla ya sh.milioni 10 zilipatikana.

Baadhi ya wahitimu wa Kidato cha Sita wakiimba ngojera wakati wa sherehe za mahafali ya kidato cha sita. (FULL SHANGWA)(FS)

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akiwasili Shuleni hapo.


Mwenyekiti
wa Bodi ya Shule ya Sekondari Kibosho, Mhandisi Aloyce Peter
Mushi akizungumza wakati wa hafla ya mahafali ya Kidato cha Sita ya
Shule ya Sekondari ya Kibosho. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akizindua jengo la mahabara ya Shule ya Sekondari Kibosho,
wakati wa mahafali ya 30 ya kidato cha sita yaliyofanyika
Mkoani Kilimanjaro. Kushoto ni Mkuu wa Shule hiyo, sista Anna na kulia
ni Mwenyekiti wa Bodi ya shule hiyo, Mhandisi Aloyce Peter Mushi. Benki
ya CRDB ilitoa mchango wa shs. milioni 5 kwa ajili ya shule hiyo.

Mkurugenzi
Mtendaji wa Benki ya CRDB Dk. Charles Kimei akizindua gazeti la shule.
Kushoto ni Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Kibosho, Sista
Anna na Mwenyekiti wa Bodi ya Shule, Mhandisi Aloyce Peter Mushi.