BABA WA EMMY KOSGEI ALIFIKISHA SHIRIKA LA NDEGE POLISI KWA KUNYANYASWA NA ULEMAVU WAKE
Askofu Kosgei na bintiye Emmy nyuma yake wakati wa uzinduzi wa album ya nne ya Emmy huko Eldoret nchini Kenya, pembeni ni wahudumu ...
http://samchardtz.blogspot.com/2014/05/baba-wa-emmy-kosgei-alifikisha-shirika.html
![]() |
| Askofu Kosgei na bintiye Emmy nyuma yake wakati wa uzinduzi wa album ya nne ya Emmy huko Eldoret nchini Kenya, pembeni ni wahudumu wa shirika la ndege la Fly540.©nairobinews |
Askofu Jackson Kosgei wa kanisa la Worldwide Gospel la nchini Kenya ambaye ni baba wa mwimbaji nyota wa muziki wa injili nchini Kenya Emmy Kosgei mwenye ulemavu wa miguu, amefikisha malalamiko yake kwa jeshi la polisi nchini humo akidai kunyanyaswa na wahudumu wa ndege ya Fly540 baada ya kumkatalia kumsaidia kushuka kwenye ndege na kumlazimisha kushuka kutoka kwenye ndege kwa kutambaa.
Kwa mujibu wa askofu Kosgei ambaye alikuwa amepanda ndege hiyo akitokea nyumbani kwao Eldoret kwenda jijini Nairobi. Amesema baada ya dakika 40 akiwa amesimama ndani ya ndege katika uwanja wa Jomo Kenyatta bila msaada wowote, wahudumu wa ndege hiyo wakamtaka askofu huyo kushuka kwa kutambaa ili hali wakijua kwamba anaulemavu na anahitaji msaada.
Kwa mujibu wa mtandao wa nairobinews umeandika kwamba askofu Kosgei alifungua jalada namba OB no 18/11/5/2014 katika kituo cha polisi cha uwanjani hapo akieleza kwamba wahudumu hao walikataa kumsaidia hata kwa kuomba mtu yeyote kumsaidia na kutakiwa kushuka katika ndege hiyo.
