AFYA: DALILI ZA KUSAMBAA KWA KANSA YA MATITI
http://samchardtz.blogspot.com/2014/05/afya-dalili-za-kusambaa-kwa-kansa-ya.html
Wiki
iliyopita tuliendelea kueleza matatizo ya kansa ya matiti, leo
tunaelezea dalili za kusambaa kwa saratani hii mwilini.Kitendo cha kansa
kusambaa mwilini kupitia mkondo wa damu na limfu huitwa metastasis.

Kusambaa
kwa saratani hadi kwenye viungo na tishu muhimu kama vile ubongo, ini,
mifupa au mapafu bado kunaufanya ugonjwa huo kuwa hatari.
Dalili za
saratani kusambaa mwilini ni maumivu ya mifupa, maumivu kwenye titi,
vidonda kwenye ngozi, kuvimba mkono karibu na eneo la saratani na
kupungua uzito.
Pia mgonjwa huweza kuhisi dalili tofauti kwa kutegemea saratani ya matiti imesambaa kwenye kiungo gani mwilini.
Kwa mfano
saratani ya matiti iliyosambaa kwenye ini inaweza kusababisha mwili
kuwa manjano, kuongezea kiwango cha enzymes katika ini, kukosa hamu ya
kula, kichefuchefu na kutapika.
Takwimu
zinaonyesha kuwa, asilimia 70 ya wagonjwa wenye kusumbuliwa na saratani
ya matiti, hupatwa na saratani iliyosambaa kwenye mifupa.
Hii ni katika hali ambayo asilimia 10 huweza kupata saratani ya matiti iliyosambaa kwenye ubongo.
Kwa
bahati mbaya tiba nyingi za kansa ya matiti hushindwa kupenya kwenye
ubongo kwa hivyo huwa kuna uwezekano ugonjwa huo ukadhihirika tena
katika mfumo wa kati wa fahamu.
USHAURI
Licha ya
ugonjwa wa kansa ya matiti kuwa hatari mno kwa maisha yetu hasa
wanawake, lakini aina hii ya saratani inaweza kutibiwa, iwapo tu
tutaweza kuigundua mapema kwa kuwa na mazoea ya kuchunguza dalili za
kansa ya matiti katika miili yetu.
