Flatnews

Mchungaji Rwakatare Kuwatoa Wafungwa Wengiine 43 gerezani kwa Kuwalipia Faini Zao

Mchungaji  Kiongozi wa Kanisa la Assemblies of God (Mlima wa Moto), Getrude Rwakatare amesema ataendelea na mpango wake wa kuwanusuru waf...


Mchungaji  Kiongozi wa Kanisa la Assemblies of God (Mlima wa Moto), Getrude Rwakatare amesema ataendelea na mpango wake wa kuwanusuru wafungwa wanaotumikia adhabu magerezani kwa kuwalipia faini ili warejee uraiani.

Akizungumza na waandishi wa habari jana Dar es Salaam, alisema katika awamu ya pili ameamua kuwalipia wafungwa 43 waliopo katika magereza ya Mkoa wa Dodoma.

“Kampeni hii ya kuwalipia faini kati ya Sh 50,000 hadi 200,000 wafungwa waliopo magerezani imetupa moyo na Watanzania wengi wameguswa na hata kutupongeza. Kutokana na hali hii kanisa letu sasa limefanya hivyo tena na safari hii tunaelekea mkoani Dodoma,” alisema.

Mchungaji Rwakatare alisema kesho watawatoa wafungwa hao mkoani Dodoma ambapo vigezo walivyoangalia ni wanawake wanaonyonyesha, wagonjwa na wazee.

“Nasi tunatimiza maandiko ya Mungu katika kufanya hivi na kuunga mkono juhudi za Mwenyekiti wa Parole, Augustino Mrema,” alisema Mchungaji Rwakatare.

Alisema kutokana na makosa mbalimbali ya faini waliohukumiwa nayo wafungwa hayo, kanisa lao limetoa Sh milioni 6.8 kwa ajili ya kulipia faini hizo.

Awali Rwakatare kupitia kanisa lake, aliwalipia wafungwa 78 katika magereza matatu ya Keko, Segerea na Ukonga ya jijini Dar  es Salaam na kuachiwa huru baada ya kulipa faini ya Sh milioni 25 zilizochangwa na waumini wa kanisa hilo.

Related

NEWS 2856764726633734906

Post a Comment

emo-but-icon
:noprob:
:smile:
:shy:
:trope:
:sneered:
:happy:
:escort:
:rapt:
:love:
:heart:
:angry:
:hate:
:sad:
:sigh:
:disappointed:
:cry:
:fear:
:surprise:
:unbelieve:
:shit:
:like:
:dislike:
:clap:
:cuff:
:fist:
:ok:
:file:
:link:
:place:
:contact:

Hot in weekRecentComments

Recent

Kesi ya Godbless Lema na mkewe kumtukana Mkuu wa Mkoa wa Arusha yakwama kusikilizwa..

Kesi ya kumtukana Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo, inayomkabili Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini, Godbless lema na mke wake Neema Lema (33), imeshindwa kusikilizwa maelezo ya awali. Hatu...

PICHA 18: Style za nywele za baadhi ya mastaa wa muziki Nigeria

              Mastaa wa muziki ni watu ambao wanapenda kwenda na fashion kuanzia mavazi mpaka style za unyoaji. Kwa upande wa mastaa wa Nigeria tumez...

Donald Trump Akataa Kulipwa Mshahara wa Urais

Rais mteule wa Marekani, bilionea Donald Trump amesema hatakubali kupokea mshahara wa urais pindi atakapokuwa madarakani. Trump ameweka msimamo huo jana katika mahojiano maalum na mtangazaji maa...

Jealousy!!! Justine Skye can't stand seeing Wizkid with other girls

As much as we know, Wizkid and Justice Skye are together. Maybe not a great deal. But, at least, there's something going on with the two. To further prove the possibility of the two being deeply in...

Comments

Anonymous:

Hahahaha Safi sana nidhamu ikae Pahala pake

item