JESHI LA POLISI TZ NDIYO LINAMTAMBUA LOWASSA KUWA NI NANI NCHINI, CHAMOTO WAKIONA SASA NA AMETOA AGIZO KALI SANA
ALIYEKUWA mgombea Urais wa Chadema, Edward lowassa, amelitaka jeshi la Polisi nchini kuwachukulia hatua wale wote wanadaiwa kumuua, aliy...
https://samchardtz.blogspot.com/2015/11/jeshi-la-polisi-tz-ndiyo-linamtambua.html
ALIYEKUWA mgombea Urais wa Chadema, Edward lowassa, amelitaka jeshi la
Polisi nchini kuwachukulia hatua wale wote wanadaiwa kumuua, aliyekuwa
Mwenyekiti wa chama hicho mkoa wa Geita, Alphonce Mawazo na kwamba kama
hawatafanya hivyo, watachukua hatua wao wenyewe.Anaandika Moses Mseti, Mwanza … (endelea).
Kauli hiyo ameitoa ikiwa ni siku mbili sasa tangu Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza, kutoa hukumu kwa chama hicho kikuu cha upinzani kumuaga na kumzika Marehemu Mawazo bila kuingiliwa na mtu yeyote.
Marehemu Mawazo, alifariki Novemba 14 mwaka katika kijiji na kata ya
Katoro, wilaya na Mkoa wa Geita na watu wanaosadikiwa kuwa ni wafuasi wa
CCM.
Lowassa ametoa kauli hiyo leo wakati akitoa salamu za rambirambi katika
ibada ya kuaga mwili wa Mawazo kwenye uwanja wa Furahisha jijini Mwanza.
Lowassa ambaye alikuwa mgombea wa Chadema na kuungwa mkono na vyama vya
Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) amesema polisi wasipochukua hatua
kwa waliomuua marehemu Mawazo watajichukulia hatua wao.
Amesema kuwa watu waliomuua Mawazo wanafahamika majina yao lakini Polisi
kwa kushirikiana na Chama cha Mapinduzi (CCM) wameshindwa kuwachukulia
hatua zozote zile mpaka sasa.
“Hawa Polisi wanafanya mambo yao kiimra-imra, kiujanja ujanja, wao
wameleta magari ya washawasha yaliyonunuliwa kwa Dola za Kimarekani 282
milioni, hawana nama ya kuyatumia, wameamua kuwachokoza wananchi ili
waweze kuyatumia.
“Wananchi nawaomba sisi tuache vurugu ili sasa hayo magari yao
walionunua tuone watakavyo yatumia, wananua magari alafu shuleni hakuna
madawati na barabara hakuna,” amesema Lowassa.
Pia amesema baada ya Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza kutoa haki kwa familia
na chama hicho kumuaga Mawazo, imeonekana jeshi la polisi halina
intelejensia wanayodai bali ni waongo watupu.
Lowassa amesema hukumu ya Jaji Lameck Mlacha wa Mahakama Kuu, iwe somo
kwa polisi wa Tanzania kutokana na kujawa wivu usiofahamika.
Freeman Mbowe
Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe, akizungumza katika shughuli
hiyo ya kuaga mwili huo, amesema haki imepatikana mahakamani na
kuwaumbua polisi.
“Wananchi wamechoka kuuliwa kama ilivyotokea kwa wafuasi wa Chadema
tangu mwaka 2011 mpaka sasa wakati huu wa Mawazo…tumechoka kufa, mwenye
akili na afahamu,” amesema Mbowe.
Hata hivyo, amesema wapo baadhi ya askari polisi wema na wenye
kutekeleza weledi wa kazi zao kiufasaha, lakini wapo ambao hawafai
kuwatumikia na kuwaongoza wananchi.
Aidha, aliwashukuru watu wote waliojitolea kuisaidia familia ya Marehemu
Mawazo hasa mtoto wake Precious Mawazo (9) anayesoma darasa la nne
akiwamo Lowassa pamoja na wabunge 113 wanaotoka vyama vya Ukawa, kwa
kila mmoja kujitolea Sh. 300,000 na kupatikana 36 milioni.
Katika hatua nyingine, Mbowe amesema chama hicho kinajiandaa kumfungulia
mashitaka ya madai Kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza, Charles Mkumbo,
baada ya kuweka zuio la mwili wa Mawazo kutoagwa jijini Mwanza hadi
Mahakama Kuu ilipotupilia mbali zuio hilo.
“Kamanada Mkumbo lazima alipe gharama zote za siku nane za kumweka
Lowassa, Sumaye, Mbowe na wabunge zaidi ya 50 jijini Mwanza wakisubiri
mahakama itende haki na hatimaye kushinda kesi,” amesema mwenyekiti
Mbowe.
Frederick Sumaye
Waziri Mkuu mstaafu wa serikali ya awamu ya tatu, Frederick Sumaye,
amesema nchi yetu awali ilikuwa inasifiwa kwa amani na utulivu, lakini
sasa inawaua watu wanaodai haki.
“Hii ni kama ilivyokuwa Afrika Kusini wakati wa utawala wa Makaburu,
mpigania haki Steve Bicco, aliuawa kama alivyouawa Mawazo, lakini mwisho
wake makaburu hao walitoa haki kwa waliowengi licha ya kuwa na bunduki
na polisi wengi kuliko kwetu,” amesema Sumaye.
Sumaye amesema Marehemu Mawazo alikuwa akidai haki majukwaani, lakini
watu waliotaka kudaiwa haki waliamua kumuua huku vyombo vya dola
vikipindapinda ili haki isipatikane kwa amani.
“Lazima tusimamie amani na tupinge kuonewa maana ipo simu moja watu watachoka kuonewa kama ilivyo sasa,” amesema.
Mtoto wa Mawazo
Mtoto wa marehemu Mawazo, Precious Mawazo (9), amesema waliomuua baba
yake hawajakatisha ndoto yake ya kuwa mwanasiasa kwani siku moja atakuwa
mwanasiasa mkubwa.
“Wakati wa uhai wa baba, ndoto yangu ilikuwa niwe mwanasiasa, lakini
nitaendelea na hiyo ndoto hadi niwe mwanasiasa mkubwa nchini…katuacha na
mdogo wangu akiwa na miaka miwili tunaamini Mungu atatusaidia,” amesema
Precious.
Godbless Lema
Godbless Lema wa Arusha akitoa salamu za rambirambi uwanjani hapo,
amesema marehemu Mawazo alikuwa rafiki yake wa damu tangu akiwa jijini
Arusha na kumshawishi kuingia kwenye siasa, lakini aliuliwa kinyama na
watu wasiopenda haki.
Lema amesema ukimya wa wananchi katika mauaji wanayofanyiwa, si uoga
bali ni unatokana na uchungu walionao, kwani wauaji wakiwa huru hakuna
atakayekuwa salama.
Mchungaji Swai
Mchungaji Bernard Swai wa kanisa la Winners jijini Mwanza, akihubiri
katika misa ya kumuaga, amesema wanadamu hawajumbwa na Mungu kwa ajili
ya kuuana bali kupendana.
“Lazima wanadamu wajiulize kwanini vijana wengi wanatumiwa ili kuwaua
wengine, tunaiomba serikali iliyopo madarakani isimamie na kukomesha
kabisa mauaji yasiyo na hatia,” amesema Mchungaji Swai.
Amesema damu ya Mawazo inalia mbele ya Mungu na wale waliofanya kitendo
cha kinyama kwa mtu huyo macho ya Mungu yanamuona popote alipo.
Hata hivyo wengine waliotoa salamu za rambirambi ni Baraza la Vijana
Taifa (Bavicha), Baraza la Wanawake (Bawacha) na chama cha NCCR Mageuzi
kilichosimama kuwakilisha vyama vinavyounda Ukawa (CUF na NLD).