MASHABIKI WA LIVERPOOL WAMTUPIA MATUSI JOE GOMEZ KISA WAYNE ROONEY
Beki wa Liverpool Joe Gomez hivi karibuni amepata majanga ya kupokea matusi mengi kutoka kwa mashabiki wa kwenye club yake ya Liverpool...
https://samchardtz.blogspot.com/2015/09/mashabiki-wa-liverpool-wamtupia-matusi.html
Beki wa Liverpool Joe Gomez hivi karibuni amepata majanga ya kupokea matusi mengi kutoka kwa mashabiki wa kwenye club yake ya Liverpool. Kilichotokea ni kwamba Gomez ali-tweet kumpa hongera Wayne Rooney kwa kufikisha magoli 5o kwenye timu ya taifa ya England.
Baada ya hapo mashabiki wa Liverpool wakaanza kumtukana kisa anampa sifa Rooney ambae ni mchezaji wa Man United. Jumamosi hii Manchester watacheza dhidi ya Liverpool basi upinzani umeanza mapema.
Mashabiki wengine walifikia hatua ya kusema kwamba bora asipangwe kwenye mechi, namba yake apewe mchezaji mwingine. Baada ya matusi kuwa mengi ikabidi Gomez afute tweet yake. Japokua mashabiki wengine walikua against hicho kitendo, wengi wao walikua wanamshambulia kama hii tweet hapo chini.
