KOCHA WA SIMBA AKATAA MECHI YA KIRAFIKI…ATOA SABABU ZAKE ZA KUFANYA HIVYO
Dylan Kerr kocha mkuu wa Simba SC Wakati homa ya pambano la watani wa jadi kati ya Simba na Yanga ikiwa inazidi kupamba moto mechi it...
https://samchardtz.blogspot.com/2015/09/kocha-wa-simba-akataa-mechi-ya.html
Dylan Kerr kocha mkuu wa Simba SC
Wakati homa ya pambano la watani
wa jadi kati ya Simba na Yanga ikiwa inazidi kupamba moto mechi
itakayopigwa kwenye uwanja wa taifa siku ya Jumamosi.
Kiongozi wa klabu hiyo Abdul
Mshangama amesema kocha kocha mkuu wa timu hiyo Dylan Kerr amekataa
kucheza mchezo wa kirafiki kabla ya kuwavaa Yanga lakini pia akieleza
hali ya kambi huko visiwani Zanzibar.
“Kocha ameamua tusicheze mechi
yoyote ya kirafiki ili kuwajenga wachezaji kisaikolojia na kufanya
mazoezi, utakuta asubuhi tunafanya mazoezi kwa masaa matatu halafu jioni
tunaenda kwenye fukwe za Zanzibar kwahiyo hakuamua wachezaji wacheze
mchezo wa kirafiki akihofia ‘injuries’”, amesema Mshangama.
“Kambi inaendelea vizuri na
wachezaji wote wako katika hali nzuri, Banda jana amefanya mazoezi
kwenye ‘session’ zote mbili. Morali iko juu sana na wachezaji wanatamani
siku hiyo ifike tucheze na watani wetu wa jadi naamini mchezo utakuwa
mzuri sana”.
