BAHANUZI, JAVU, KUIVAA STAND JUMAMOSI WAKIWA KWENYE KLABU YAO YA ZAMANI
Mabingwa wa zamani wa ligi kuu Tanzania baratimu ya Mtibwa Sugar, imewarejesha kundini ‘mastraika’ Said Bahanunzi na Hussein Javu a...
https://samchardtz.blogspot.com/2015/09/bahanuzi-javu-kuivaa-stand-jumamosi.html
Mabingwa wa zamani wa ligi kuu
Tanzania baratimu ya Mtibwa Sugar, imewarejesha kundini ‘mastraika’
Said Bahanunzi na Hussein Javu ambao walifanya vizuri katika klabu hiyo
kabla ya kutimkia Yanga SC.
Bahanunzi alifunga mabao nane
msimu wa 2011/12 kisha akasajiliwa Yanga, Javu akachukua nafasi yake na
kuwa mfungaji namba moja katika timu hiyo msimu wa 2012/13 naye
akatimkia Yanga mara baada ya kumalizika kwa ligi.
Baada ya kuwapoteza washambuaji
Jamal Mnyate aliyemaliza mkataba wake na kujiunga na Mwadui FC ya
Kahama, Musa Hassan Mgosi aliyejiunga na Simba SC, kocha mkuu wa timu
hiyo, Mecky Mexime amesema kuwa washambuaji hao watafanya vizuri
kushirikiana na vijana kama Ally Shomari kuifanya Mtibwa kuwa ‘moto’
msimu huu.
“Ni kweli tumewasaini Javu na
Bahanunzi kwa kuwa ni wachezaji wenye uwezo wa kuisaidia timu yetu”
amesema Mecky Mexime ambaye kikosi chake kitawavaa Stand United katika
mchezo wa ufunguzi wa ligi kuu bara siku ya Jumamosi katika uwanja wa
Kambarage, Shinyanga.
“Tulipoteza michezo miwili katika
uwanja wa Kambarage msimu uliopita (dhidi ya Kagera Sugar na Stand)
tumejiandaa kuwakabili Stand. Timu ipo vizuri naimani tutaanza msimu
vizuri”.
Anaongeza kusema Mecky ambaye pia
amemrejesha mlinda lango aliyeshindwa kutulia Simba SC, Hussein
Sharrif. Mtibwa iliifunga Stand 3-1 katika mchezo wa kwanza msimu
uliopita lakini ikachapwa 1-0 katika uwanja wa Kambarage katika gemu ya
marejeano.
