SPUTANZA YAIVALIA NJUGA YANGA KUHUSU KASEJA
Chama cha Wacheza soka Tanzania SPUTANZA, kimewasilisha barua kwa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kulitaka limtangaze mlinda...
https://samchardtz.blogspot.com/2015/08/sputanza-yaivalia-njuga-yanga-kuhusu.html
Chama cha Wacheza soka Tanzania SPUTANZA, kimewasilisha barua kwa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kulitaka limtangaze mlinda mlango Juma Kaseja kuwa ni mchezaji huru.
Kaseja ambae Yanga imemfungulia
mashtaka kwenye mahakama ya kazi ikitaka mchezaji huyo kuwalipa
mamilioni ya shilingi wakimtuhumu kuvunja mkataba na timu hiyo.
Mwenyekiti wa SPUTANZA Mussa Kisoky amesema, tayari wameshapeleka barua TFF wakiomba imtangaze Kaseja kama mchezaji huru.
“Ni kweli Juma alikuja kwenye
chama, alileta malalamiko yake kuhusu Dar Young Africans na sisi
tumeshaanza kulishughulikia suala lake, tumelipeleka TFF tayari kwahiyo
sisi ombi letu kwa TFF ni kuwaambia wamtangaze Juma kama mchezaji huru
kutokana na taratibu zilizokuwa zimefanyika hazikufata mstari ule
unaotakiwa kwenye system ya soka”, amesema Kisoky.
Awali Juma aliwaandikia Yanga
barua ya kuvunja mkataba baada ya Yanga kutotekeleza baadhi ya vifungu
vya mkataba hasa kipengele kinachohusu ada ya usajili ambapo Yanga
walikuwa wamekiuka makubaliano na yeye akaamua kuvunja mkata. Lakini
wakati anafanya hivyo, tayari Yanga walikuwa wamemuwekea pesa kwenye
akaunti yake.
Lakini ikumbuikwe kuwa, Yanga
kupitia kwa mwanasheria wao Frank Chacha ilishasema Kaseja yuko huru
kujiunga na klabu yoyote akisema kwamba, wanachokitaka Yanga kutoka kwa
Kaseja ni madai yao ya kuvunjwa kwa mkataba, “Yanga imeshazungumza na
golikipa huyo pamoja na wakili wake kwamba akitaka barua ya kuondoka
Yanga ‘release letter’ wao wako tayari kumpatia lakini suala la kesi
litabaki palepale”, alisema Chacha miezi kadhaa iliyopita.
