Flatnews

SIMBA NAYO YASAJILI MZIMBABWE HUYU….

Katika hali ya kuendelea kuimarisha kikosi chao kwa ajili ya mchakamchaka wa ligi kuu msimu ujao timu ya Simba SC leo imeshusha kifaa k...


Katika hali ya kuendelea kuimarisha kikosi chao kwa ajili ya mchakamchaka wa ligi kuu msimu ujao timu ya Simba SC leo imeshusha kifaa kingine kutoka Zimbabwe akiwa ni kiungo mshambuliaji Justice Majabvi ambae tayari ameanza mazoezi na kikosi cha msimbazi kilichopiga kambi yake visiwani Zanzibar kwa ajili ya kufanya mazoezi kujiweka tayari na
msimu ujao wa ligi.
Kiongozi wa kambi ya Simba visiwani Zanzibar Abuli Mshangama amesema tayari mchezaji huyo ametua Zanzibar akitokea Vietnam lakini hajasema mchezaji huyo wamemsajili kwa mkataba wa miaka mingapi.
Katika hatua nyingine, ‘Wekundu wa Msimbazi’ jana usiku walitoa kipigo kingine visiwani Zanzibar ambapo waliilaza timu ya Polisi kwa goli 2-0 kwenye pambano lililofanyika kwenye uwanja wa Amaan.
Magoli ya Simba yamefungwa na Elias Maguri pamoja na Mussa Hassan ‘Mgosi’,  Simba itaendelea na ratiba ya kucheza mechi zake za kirafiki ikwa visiwani Zanzibar ambapo Jumatatu itakutana na Jang’ombe Boys na mechi yao ya mwisho ya kirafiki itachezwa dhidi ya KMKM ambayo imetoka kwenye michuano ya Kagame siku chache zilizopita.

Related

SPORTS 7183492284056520411

Post a Comment

emo-but-icon

item