Flatnews

SERIKALI YA TANZANIA YAITUNUKU HUAWEI TUZO YA UONGOZI BORA NA MCHANGO MKUBWA KATIKA SEKTA YA TEKNOLOJIA NA MAWASILIANO

Mkuu wa masuala ya ufumbuzi na ushauri wa Huawei Afrika mashariki na kusini Dr. Bello Moussa, akizungumza wakati wa mkutano wa sik...


Mkuu wa masuala ya ufumbuzi na ushauri wa Huawei Afrika mashariki na kusini Dr. Bello Moussa, akizungumza wakati wa mkutano wa siku mbili wa kimataifa ulipewa jina la Connect to Connect (C2C) ulioandaliwa na Wizara ya Mawasiliano na teknolojia kujadili changamoto za mawasiliano pamoja na ukuaji wa broadband katika nchi za Afrika. Mkutano ulifanyika katika hoteli ya kimataifa ya Ramada Resort jijini Dar es Salaam.
Meneja Uhusiano Huawei Tanzania Bw. Jimmy Nlinguo akipokea tuzo ya uongozi bora kutoka kwa Kaimu Katibu Mkuu, Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Selina M. Lyimo kutokana na mchango mkubwa wa kampuni hiyo katika sekta ya teknolojia na mawasiliano hapa nchini. Tuzo hiyo ilitolewa wakati wa mkutano wa siku mbili wa kimataifa wa Connect to Connect (C2C) ulioandaliwa na wizara hiyo katika hoteli ya kimataifa ya Ramada Resort jijini Dar es Salaam kujadili changamoto za mawasiliano pamoja na jinsi ya kuongeza ukuaji wa broadband katika nchi za Afrika.
Meneja Uhusiano wa Huawei Tanzania akisema maneno machache ya shukrani kwa wadau wa sekta ya mawasiliano na teknolojia mara baada ya kampuni yake kutunikiwa tuzo ya uongozi bora na Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia kutokana na mchango mkubwa wa kampuni hiyo katika sekta ya teknolojia na mawasiliano hapa nchini. Tuzo hiyo ilitolewa wakati wa mkutano wa siku mbili wa kimataifa wa Connect to Connect (C2C) ulioandaliwa na wizara hiyo katika hoteli ya kimataifa ya Ramada Resort jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa masuala ya ufumbuzi na ushauri wa Huawei Afrika Mashariki na kusini Dr. Bello Moussa, akijibu maswali ya waandishi wa habari muda mfupi baada ya kutoa hotuba yake kwenye mkutano wa kimataifa uliondaliwa na wizara ya mawasiliano, sayansi na teknolojia uliopewa jina la “Connect to Connect (C2C)” uliofanyika katika hoteli ya kimataifa ya Ramada Resort jijini Dar es Salaam.
Meneja Uhusiano wa Huawei Tanzania akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kampuni yake kutunikiwa tuzo ya uongozi bora na Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia kutokana na mchango mkubwa wa kampuni hiyo katika sekta ya teknolojia na mawasiliano hapa nchini. Tuzo hiyo ilitolewa wakati wa mkutano wa kimataifa wa Connect to Connect (C2C) uliofanyika katika hoteli ya Ramada jijini Dar es salaam.

Kampuni inayongoza katika sekta ya teknolojia na mawasiliano nchini Tanzania (Huawei) imetunikiwa tuzo ya uongozi bora kutokana na mchango wao mkubwa sekta ya teknolojia na mawasiliano hapa nchini.

Tuzo hiyo imetolewa siku ya jana katika hoteli ya kimataifa ya Ramada jijini Dar es salaam ambapo mkutano wa kimataifa wa siku mbili unaendelea. Wizara ya mawasiliano na teknolojia huadhimisha mkutano huo kila mwaka kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa sekta hiyo.


Mkutano huo umewaleta pamoja wadau katika sekta ya teknolojia na mawasiliano, watunga sera, wawekezaji pamoja na wafumbuzi mbalimbali kwa nia ya kujadili mbinu za kukuza teknolojia ya ‘Broadband’ kati ya nchi na nchi barani Afrika, kutoka pwani hadi pwani na uvumbuzi utakaosaidia kusukuma uchumi wa Tanzania na kukuza ubora wa huduma za jamii.

Huawei walipokea tuzo hiyo kutoka Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia baada ya kuwa mstari wa mbele katika sekta ya teknolojia sayansi na mawasiliano pamoja na kuwa kiongozi katika utafiti na kuchangia katika ukuaji na usambazaji wa teknolojia ya broadband nchini Tanzania.

Akizungumza wakati wa mkutano huo, Mkuu wa masuala ya ufumbuzi na ushauri wa Huawei Afrika  Mashariki na Kusini, Dr. Bello Moussa alisema “ Nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika katika miaka ya hivi karibuni zimeonyesha shauku kubwa kwenye kuwekeza na kukuza teknolojia ya broadband. Changamoto ni kwamba nchi hizi zipo katika hatua tofauti ya maendeleo ya teknolojia ya taarifa na mawasiliano na kwa bahati mbaya asilimia 90 ya wananchi wake bado hawajapata huduma hii ya broadband majumbani mwao na hivyo wako nyuma ukilinganisha na masoko yaliyoendelea.”

Huawei walitumia mkutano huo pia kutambulisha mtandao wake wa LTE ambao umepewa jina la “Mkakati wa Huawei kuelekea 5G”. Wakati wa utambulisho huo, Huawei iliweka bayana mchakato mzima wa kuhama kutoka 3G kwenda 4G/4.5G hadi 5G.

Kuhamia kwenye teknolojia ya LTE ni kuongeza ushindani. Teknolojia ya LTE inazidi kukomaa baada ya teknolojia hiyo kusambaa kwenye mitandao. Akitambulisha mtandao mpya wa 5G wakati wa warsha ya ‘Connect to Connet’ (C2C) ambayo pia ilidhaminiwa vilivyo na kampuni ya Huawei Tanzania, Makamu wa Rais wa Huawei ‘Wireless marketing’, Alex Wang alisema “Huawei wamesaidia ujenzi wa mitandao karibia 200 ya LTE dunia nzima na kujizolea uzoefu wakutosha katika mageuzi ya mitandao ya simu.

Huawei inaendelea kuwa makini katika kulinda uwekezaji wa wateja wake na muhimu zaidi kulenga katika ukuaji na mageuzi ya mitandao ili kusaidia wateja wake kuongeza ushindani”.

Mchango wa Huawei katika utafiti wa 5G umetambulika katika sekta nzima na ndio maana wakatunukiwa tuzo ya “Mchango bora katika maendeleo ya 5G” katika warsha ya LTE iliyofanyika Amsterdam, Uholanzi wakati wa mkutano wa dunia wa 5G tarehe 26 June 2015.

Hii pia ni mara ya pili kwa serikali ya Tanzania kutambua mchango na jitihada za Huawei nchini ambapo licha ya tuzo ya jana ni pamoja na Huawei kutimiza makubaliano ya mkataba kati yake na serikali  juu ya  mchakato wa teknolojia na mawasiliano ili kutimiza malengo ya nchi ifikapo mwaka 2025.

Related

NEWS 2810272770320898755

Post a Comment

emo-but-icon

item