Flatnews

Wavuvi waagizwa kutowasaidia wahamiaji

Wahamiaji wa kabila la Rohingya waliookolewa na wavuvi Wavuvi kutoka Indonesia wamesema kuwa wameamr...


Wahamiaji wa kabila la Rohingya waliookolewa na wavuvi
Wavuvi kutoka Indonesia wamesema kuwa wameamriwa na Serikali kuwa wasiwalete wahamiaji wanaopatikana wakielea kwenye vyombo baharini wasiokuwa na chakula au maji ya kutosha.

Maelfu ya wahamiaji wanadhaniwa kuwa wanaelea Baharini katika maeneo karibu na Indonesia, Thailand na Malaysia.Baadhi ya wahamiaji waliookolewa na wauvuvi Indonesia
Licha ya wito wa Umoja wa Mataifa kuwa wahamiaji waruhusiwe kufika ufuoni, mataifa hayo matatu yamefukuza boti zilizojaa wahamiaji.
Ni wale watu wanaojitahidi kufika nchi kavu pekee wanaoruhusiwa katika nchi hizo.wavuvi wa Indonesia
Wahamiaji wengi ni Waislamu wa jamii ya Rohingya wanaotoroka mateso nchini Mynamar.
Watu wengi wanataka taifa la Myanmar kuchukua wajibu mkubwa zaidi kuhusiana na wahamiaji hao lakini taifa hilo limekataa likidai kuwa halipaswi kulaumiwa kwa hali hiyo.
CHANZO NI BBC SWAHILI

Related

NEWS 505245120325407236

Post a Comment

emo-but-icon

item