Flatnews

UPASUAJI WA FIZI WA WAMKOSESHA HAZARD SHEREHE YA KUKABIDHIWA TUNZO

Nyota wa Chelsea Eden Hazard alishindwa kuhudhuria sherehe ambapo alitakiwa kutunukiwa tuzo ya mchezaji bora msimu kwa waandishi ...



Nyota wa Chelsea Eden Hazard alishindwa kuhudhuria sherehe ambapo alitakiwa kutunukiwa tuzo ya mchezaji bora msimu kwa waandishi wa habari baada ya kuwa
akiuguza majeraha yake yaliyotokana na upasuaji wa fizi aliofanyiwa hivi karibuni.
Hazard ambaye alijinyakulia kura za kutosha kutoka kwa waandishi, huku akipata asilimia 53 na kumzidi Harry Kane wa Tottenham ambaye alishika nafasi ya pili, alitakiwa kukabidhiwa zawadi yake katika sherehe zilizofanyika jijini London.
"Shukrani za dhati ziwafikie Waandishi wa Habari za Michezo nchini Uingereza kwa kunichagua kuwa mchezaji wao wa msimu. Naomba radhi kuwa sitaweza kuhudhuria usiku huu mahala hapo lakini tafadhali mnatakiwa kufahamu kuwa ninajivunia sana juu ya hii zawadi ambayo kwangu mimi ni kubwa sana," aliandika hivyo kwenye ukurasa wake wa Twitter.

Related

SPORTS 2290891470355697110

Post a Comment

emo-but-icon

item