ACT Wazalendo kuibukia Operesheni Maji maji
Kiongozi wa chama cha ACT wazalendo Zitto Kabwe (katikati) akishauriana ja...
https://samchardtz.blogspot.com/2015/05/act-wazalendo-kuibukia-operesheni-maji.html

Kiongozi wa chama cha ACT wazalendo Zitto Kabwe (katikati) akishauriana jambo na Katibu mkuu Samson Mwigamba.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Afisa Habari ACT Wazalendo Abdallah Khamis imebainisha kuwa Lengo la operesheni maji maji litakuwa kukagua uhai wa chama kazi itakayofanyika kwa siku 12 kwa timu kumi za kazi kujigawa katika maeneo mbali mbali.
Hayo yanafuatia kamati Kuu ya Chama cha ACT-Wazalendo, iliyokuwa na kikao chake cha kawaida cha siku mbili kilichokaa tarehe, 23 na 24 mwezi huu na kilichoongozwa na Mwenyekiti wa Taifa, Anna Mghwira, pia kilihudhuriwa na kiongozi wa Chama Zitto Zuberi Kabwe ambapo kilikuwa na ajnda za Uteuzi wa nafasi mbali mbali za kiutendaji ndani ya chama, Operesheni majimaji pamoja na Ratiba ya Uchaguzi mkuu na Ngome za Chama.
Katika mkutano kamati kuu wanachama wafuatao wameteuliwa:
Manaibu katibu wakuu bara na Zanzibar ni Msafiri, Abrahaman Mtemelwa na upande wa Zanzibar ni Juma Said Sanani, kuwa Naibu katibu Mkuu Zanzibar
Makatibu wa kamati mbalimbali, Kamati kuu imemteua Peter Mwambuja kuwa katibu wa Fedha na Rasilimali
Nafasi ya wenyeviti, Kamati kuu imemteua Estomih Mallah kuwa mwenyekiti wa Kamati ya Fedha na Rasilimali na Mwanasheria wakili Albert Msando, ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa kamati ya Katiba na Sheria
Wajumbe Wa Kamati Kuu, Kamati kuu imewateua Mzee Japhari Kasisiko na Hamad Mussa Yusuph
Kwa upande wa washauri wa chama Kamati kuu kwa nafasi yake imewateua Profesa Kitilla Mkumbo na Tery Bermunda(mama Tery) kuwa washauri wa Chama.