ZENGWE KATIKA MJENGO WA DIAMOND, LICHA KUJENGA KWA MAMILIONI
SIKU chache baada ya sehemu ya ukuta wa uzio wa mjengo wa msanii nyota wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ kuanguka, mtaalam ...
https://samchardtz.blogspot.com/2015/04/zengwe-katika-mjengo-wa-diamond-licha.html
SIKU chache baada ya
sehemu ya ukuta wa uzio wa mjengo wa msanii nyota wa Bongo Fleva, Nasibu
Abdul ‘Diamond’ kuanguka, mtaalam wa majengo aliyejitambulisha kwa jina
la Injinia Stuart Daniel ameupiga zengwe akidai licha ya kuonekana kuwa
na nakshinakshi nyingi, lakini ni dhaifu na unaweza kudondoka.
Akizungumza na Gazeti la
Amani mwanzoni mwa wiki hii baada ya nyota huyo kutupia picha za uzio
wake katika mtandao ukiwa chini kwa mwereka wa mvua, Injinia Stuart
alisema anaamini nyumba ya Diamond imejengwa chini ya kiwango na mafundi
walimchakachua simenti.
MSIKIE MWENYEWE INJINIA
“Kama jengo lote
lilijengwa kwa staili hii, basi ni suala la kusubiri kwa muda tu kabla
hatujasikia habari za kuanguka kwake na kama hatakuwa makini, linaweza
kumletea madhara makubwa. “Kitu ambacho ningeweza kumshauri ni kuwaita
wakaguzi wa majengo waangalie mafundi wake walivyojenga ili kuepuka
hasara anayoweza kuipata,” alisema mtaalam huyo.”
ACHAMBUA UJENZI ULIVYO
“Kuna kitu katika ujenzi
tunaita ratio (uwiano) kati ya mchanga wa kujengea na simenti. Huu
mchanganyiko inabidi ukamilike kutegemea urefu, unene na ukubwa wa
kinachojengwa, kitu chochote kikipungua, matokeo yake ndiyo haya,
mafuriko kidogo au tetemeko dogo tu linaweza kuporomosha jumba zima,”
alisema Injinia Daniel.
Muonekano wa ukuta huo uliobomoka.
WALICHOSEMA WANAOMJUA DIAMOND
Amani pia lilizungumza
na baadhi ya watu wa karibu wa Diamond ambao walisema kuwa, tatizo
lililomtokea staa huyo linatokana na tabia ya umaarufu.“Unajua watu
maarufu na wenye pesa, wanapojenga wanapenda sana kuwasiliana na mafundi
wao kwa njia ya simu. Utakuta mtu yupo mjini, anawasiliana na fundi
yupo saiti, fundi anaomba shilingi laki moja anunulie simenti, inatumwa
kwa njia ya mitandao ya pesa.
“Sasa hapo unategemea
nini? Fundi atatumia elfu hamsini, elfu hamsini ataweka ndani. Ndiyo
maana ukiangalia ukuta wa nyumba ya Diamond ulioanguka, nondo zilikuwa
nyembamba sana na inaonekana hata simenti ilikuwa chache kwenye
matofali,” alisema mmoja wa watu hao akiomba jina lake lisiandikwe
gazetini.
Mwingine alisema: “Ki
ukweli Diamond ‘amepigwa’ na mafundi kwenye ile nyumba. Iko haja ya
kuchukua wataalam wa majengo wakakague ili kama ni kweli mpaka matofali
yaliyotumika kujengea nyumba kubwa yako chini ya kiwango, achukue hatua.
Lakini mwenyewe anakimbilia kusema mafundi ni wawili tofauti.”
DIAMOND AULIZWA, AKIRI KUCHAKACHULIWA
Baada ya maelezo hayo
yote, Amani liliwasiliana na Diamond na kumuuliza kuhusu zengwe hilo
linalodaiwa amepigwa kwenye mjengo wake aliohamia hivi karibuni.Kwanza
alikiri suala la mafundi waliojenga awali kufanya uchakachuaji wa
kutumia simenti kiduchu na nondo zisizositahili.
“Ni kweli, wale mafundi
nimeambiwa kwa jinsi walivyojenga, walichakachua simenti. Hata hivyo,
kwa kulitambua hilo nimechukua mafundi wapya na kazi inayorudiwa sasa ni
ya uhakika zaidi. Huu ujanjaujanja uliofanyika hata mimi sijakubaliana
nao.”
Amani: “Kwa hiyo unarudia ujenzi wa nyumba yote?”
Diamond: “Aaa! No!
Unajua mafundi waliojenga ule ukuta ulioanguka siyo waliojenga nyumba
kubwa. Ni mafundi wawili tofauti. Kwa hiyo nina imani nyumba kubwa ipo
sawasawa.”
Amani: “Baadhi ya marafiki zako wanasema fundi ni mmoja ila unasema ni wawili ili usibanwe kuhusu kuirudia nyumba kubwa.”
Diamond: “Hamna bwana!
Waliojenga ukuta wa uzio siyo wa nyumba kubwa. Ndiyo maana nimewaita
wengine kujenja upya uzio. Unajua naishi kwa wasiwasi, maana kama wale
walichakachua si ipo siku unaweza kukuta ukuta wote chini na wezi
wameingia, nakuwa na wasiwasi sana.”
INJINIA ARUDIWA
Baada ya Diamond
kuzungumza hayo kuhusu mafundi wa nyumba kubwa kuwa wengine na mafundi
wa uzio, Amani lilimrudia Injinia Daniel na kumuuliza kuhusu sheria ya
ujenzi wa aina hiyo inasemaje.“Hapo sasa ni ujenzi holela! Mjenzi
anatakiwa kuwa mmoja tu. Huyohuyo wa nyumba kubwa anatakiwa amalizie na
uzio kama mtu ataamua kuweka uzio.
Nyota wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’.
“Ndiyo maana huwa
tunawataka watu wafuate sheria za kuajiri wajenzi wenye viwango vya
kisheria ili waweke na ule ubao wa maelekezo ya ujenzi.“Kwa kawaida kile
kibao kina maelezo ya; project (mradi), contractor (mjenzi), client
(mteja), consultant (mshauri), supervisor (msimamizi). Kuna mabango
mengine hadi mtoa pesa ambaye ni financier anaandikwa pia na siku ya
kuanza ujenzi na makadirio ya kumaliza.”