Mzigo kutoka Tunisia: Tazama Yanga wanavyowatafutia dawa Etoile
Katika mazoezi ya jana usiku kocha mkuu wa Yanga, Hans van der Pluijm amewaambia vijana wake ku...
https://samchardtz.blogspot.com/2015/04/mzigo-kutoka-tunisia-tazama-yanga.html
Katika mazoezi ya jana usiku kocha mkuu
wa Yanga, Hans van der Pluijm amewaambia vijana wake kujiamini na
kucheza soka la kushambulia ili kufunga magoli ya mapema na
kuwachanganya Etoile du Sahel katika mechi ya leo usiku kuanzia majira
ya saa 3:00 usiku kwa saa za Tanzania.
Mkuu wa Idara ya habari na Mawasiliano wa
Yanga, Jerry Muro naye kama kawaida yupo Tunisia kufuatilia mambo
yanavyokwenda. Yanga wanahitaji ushindi au sare ya angalau magoli 2-2
ili kusonga mbele moja kwa moja kwasababu mechi ya kwanza jijini Dar es
salaam timu hizi zilitoka sare ya 1-1
Maelekezo ya hapa na pale kabla ya kuanza mazoezi
Mrisho Ngassa (kushoto) na Simon Msuva (kulia) wanatarajia kuongoza safu ya ushambuliaji leo


