Flatnews

Wema Kamwaga Mboga, Kajala Ajiandaa Kumwaga Ugali

Baada ya siku za hivi karibuni, Wema Sepetu kuamua kumwaga mboga kwa kumfungukia shosti wake wa z...



Wema Kamwaga Mboga, Kajala Ajiandaa Kumwaga Ugali
Baada ya siku za hivi karibuni, Wema Sepetu kuamua kumwaga mboga kwa kumfungukia shosti wake wa zamani Kajala Masanja kwa kusema si rafiki mzuri na pia amefilisika, inadaiwa Kajala anajiandaa kumwaga ugali.

Rafiki wa karibu wa Kajala aliyeomba hifadhi ya jina lake, alimtonya mwandishi wetu kuwa maneno anayoyatoa Wema yanamkosesha amani mwenzake na kwamba siku si nyingi Kajala naye atajibu mapigo.
“Si unajua wale wanajuana vizuri, walikuwa wanafichiana siri zao, alipofikia Wema akae mkao wa mambo yake kuanikwa, bado Kajala anatafuta ushauri wa namna ya kujibu mashambulizi, Wema kamwaga mboga, mwenzake atamwaga ugali,” kilinyetisha chanzo hicho.
Katika kujua ukweli wa ‘ubuyu’ huu, chanzo cha hanbari hii kiifanya jitihada za kumtafuta Kajala kupitia namba yake ya simu ya mkononi lakini kila ilipopigwa haikupokelewa.

Related

B/MOVIES 4527660954586221387

Post a Comment

emo-but-icon

item