WAZIRI MIGIRO AKABIDHI NAKALA ZA KATIBA INAYOPENDEKEZWA KWA WALEMAVU, TAASISI ZA KIDNI NA ASASI ZA KIRAIA
Watanzania wametakiwa kuisoma katiba inayopendekezwa kwa umakini ili kuweza kufanya maamuzi sahihi katika kuandika historia mpy...
https://samchardtz.blogspot.com/2015/03/waziri-migiro-akabidhi-nakala-za-katiba.html
Watanzania
wametakiwa kuisoma katiba inayopendekezwa kwa umakini ili kuweza
kufanya maamuzi sahihi katika kuandika historia mpya ya nchi.
Hayo
aliyasema leo Waziri wa Katiba na Sheria,Dkt. Asha-Rose Migiro wakati
akikabidhi katiba inayopendekezwa kwa makundi mbalimbali,Migiro amesema
nchi itaandika historia mpya baada ya kupata katiba mpya.
Alisema
wananchi wakisoma katiba kwa umakini kutasaidia kufikia matarajio
katika kutengeneza ramani ya nchi kwa kuvuka miaka 50 ya katiba mpya.
Migiro
amesema kuwa wamechapisha katiba inayopendekezwa kwa watu wenye ulemavu
wa kuona kwa alama ya nukta nundu na baada ya kupita kwa katiba
watapewa kwani ni haki yao kuwa nayo.
“Kujitokeza
kwenu ni ishara ya kuunga mkono kwa katiba inayopendekezwa hivyo ni
wajibu wenu kutoa elimu ili waweze kufanya maamuzi wakati wa kupiga kura
ya maoni”amesema Dk.Asha-Rose.
Aidha
wamechapisha nakala hizo kwa herufi kubwa kwa watu wenye ulemavu wa
ngozi (Albino)ili nao waweze kusoma na kuelewa na kuweza kufanya
maamuzi.
Migiro
amesema wamechapisha nakala na kugawa kwa nchi nzima ambapo kila kata
inapata nakala 300 na Zanzibar zinagaiwa chini ya ofisi ya makamu wa
pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Idd.
Baadhi ya wadau waliopokea nakala hizo wamesema watafikisha,lakini hawawezi kuwaamulia katika maamuzi yao
Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Asha-Rose Migiro akimkabidhi nakala za Katiba
Inayopendekezwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu Dkt. Florens Turuka katika hafla fupi ya
kugawa nakala hizo kwa taasisi mbalimbali iliyofanyika katika Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es
Salaam leo (Jumatatu, Machi 16, 2015). Dkt. Turuka alipokea kwa niaba ya Makatibu Wakuu
wenzake.
Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Asha-Rose Migiro akimkabidhi nakala za Katiba
Inayopendekezwa mwakilishi wa Baraza Kuu la Taasisi na Jumuiya za Kiislam Sheikh Mussa
Kundecha katika hafla fupi ya kugawa nakala hizo zilizoandaliwa na Serikali kwa taasisi
mbalimbali iliyofanyika katika Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam leo (Jumatatu, Machi 16,
2015).
Makamu Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama vya Watu Wenye Ulemavu
(SHIVYAWATA) Bw. Amon Anastaz akisoma nakala za Katiba Inayopendekezwa mara baada ya
kukabidhiwa na Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Asha-Rose Migiro (kulia) katika hafla fupi ya
kugawa nakala hizo zilizoandaliwa na Serikali kwa taasisi mbalimbali iliyofanyika katika Ukumbi
wa Karimjee jijini Dar es Salaam leo (Jumatatu, Machi 16, 2015).
Mwenyekiti wa Chama cha Albino Tanzania Bw. Ernest Kimaya akisoma nakala za
Katiba Inayopendekezwa yenye maandishi yaliyokuzwa mara baada ya kukabidhiwa na Waziri
wa Katiba na Sheria Dkt. Asha-Rose Migiro (kulia) katika hafla fupi ya kugawa nakala hizo
zilizoandaliwa na Serikali kwa taasisi mbalimbali iliyofanyika katika Ukumbi wa Karimjee jijini
Dar es Salaam leo (Jumatatu, Machi 16, 2015).
Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Asha-Rose Migiro akimkabidhi nakala za Katiba
Inayopendekezwa mwakilishi wa Taasisi ya Mabohora Bw. Zainuddin Adamjee katika hafla fupi
ya kugawa nakala hizo kwa taasisi mbalimbali iliyofanyika katika Ukumbi wa Karimjee jijini Dar
es Salaam leo (Jumatatu, Machi 16, 2015).
Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Asha-Rose Migiro, Naibu wake Ummy
Mwalimu katika picha ya pamoja na viongozi wa taasisi za kidini katika hafla fupi ya kugawa
nakala za Katiba Inayopendekezwa zilizoandaliwa na Serikali kwa taasisi mbalimbali iliyofanyika
katika Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam leo (Jumatatu, Machi 16, 2015).
Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Asha-Rose Migiro, Naibu wake Ummy
Mwalimu katika picha ya pamoja na wawakilishi wa asasi za kiraia katika hafla fupi ya kugawa
nakala za Katiba Inayopendekezwa zilizoandaliwa na Serikali kwa taasisi mbalimbali iliyofanyika
katika Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam leo (Jumatatu, Machi 16, 2015). (Picha: Farida
Khalfan, Wizara ya Katiba na Sheria)