Matonya na Tunda Man hakuna bifu tena
Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Tunda Man
https://samchardtz.blogspot.com/2015/03/matonya-na-tunda-man-hakuna-bifu-tena.html
Wasanii wa muziki wa Bongo fleva nchini Tanzania, Matonya na Tunda Man, wamemaliza bifu lao leo baada ya kutowepo kwa maelewano baina yao ambapo kila mmoja alikuwa akimlaumu mwenzie kutokana na kazi zao za muziki.
Akihojiwa katika moja ya redio nchini Tunda Man, amesema kuwa anachohisi alimkosea Matonya, ni kusema kwamba alimtungia nyimbo lakini hataki tena kuzungumzia ishu hiyo na kuongeza kuwa leo itakuwa mara ya mwisho kuzungumzia jambo hilo na kuomba radhi kwa yote yaliyotokea, hana tatizo lolote na Matonya.
Kwa upande wake Matonya amesema kuwa Tunda Man, ni mdogo wake ambaye wamekutana vizuri na walikuwa wanaishi vizuri lakini alipata wasiwasi baada ya kuona kila siku kuna maneno yanaibuka ambayo hakupendezwa nayo, yeye binafsi anampenda sana Tunda Man, na hata familia yake, kwa nafasi yake kama kaka ameamua kumsamehe.