BreakingNews:-CHADEMA yambwaga Zitto mahakamani Kesi ya kupinga maamuzi ya chama dhidi yake yafutwa!
https://samchardtz.blogspot.com/2015/03/breakingnews-chadema-yambwaga-zitto.html
Hatimaye chama kimeshinda kesi dhidi ya aliyekuwa mwanachama wake Zitto Kabwe.
Mahakama imeamua katika hukumu yake leo kuwa Chama kinaweza kuendelea na taratibu zake. Aidha, Mahakama imeamuru Zitto alipe gharama zote za kesi.
Wanasheria wa chama, Peter Kibatala na John Mallya wataongea na Vyombo vya Habari punde.
Hongera Mwanasheria Peter Kibatala...Hongera Chadema
Haki imeshinda dhuluma ====================
Mwaka jana Zitto Kabwe aliweka pingamizi mahakamni kuzuia kikao cha Kamati Kuu kumjadili.
Hoja yake ni kupinga kuitisha kamati kuu kabla shauri lake kusikilizwa na Baraza Kuu.
Alidai anataka mahakama iagize kamati kuu ya CHADEMA kutojadili suala lake mpaka baraza kuu likae kuamua rufaa yake. Kujua chanzo cha kesi hii soma thread hii=>Zitto aweka pingamizi Mahakamani kuzuia Kikao cha Kamati Kuu kujadili rufaa yake kesho