TAMWA YATOA MAFUNZO KWA WANAHABARI WA MIKOA YA NYANDA ZA JUU KUSINI
WENCE AKITOA ELIMU KWA WANAHABARI WALIOKUTANA MKOANI IRINGA
https://samchardtz.blogspot.com/2015/02/tamwa-yatoa-mafunzo-kwa-wanahabari-wa.html
WENCE AKITOA ELIMU KWA WANAHABARI WALIOKUTANA MKOANI IRINGA
NA fredy mgunda,iringa
Waandishi
wa habari wametakiwa kuandika zaidi habari zinazohusu unyanyasaji wa
kijinsia hususan dhidi ya wanawake na watoto ili kuiamsha zaidi jamii
inayowafanyiwa vitendo hivyo na mamlaka husika ziweze kuchukua hatua za
kisheria dhidi ya vitendo hivyo.
Msisitizo
huo ulitolewa na chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania
(Tamwa) kwa waandishi wa habari wa mikoa ya nyanda za juu kusini
(IRINGA,MBEYA,SONGEA NA NJOMBE) ambapo wanahabari wameombwa kuendelea
kufichua habari hizo hususan kwa wanaofanyiwa vitendo hivyo ili waweze
kuelewa kwamba sheria dhidi ya ukatili huo zipo na kwamba kuna taasisi
za kuwatetea.
Akizungumza
wakati wa mafunzo hayo mwanahabari wa siku nyingi WENCE MUSHI alisema
dhahiri kuwa vitendo vya unanyanyasaji vimepungua kutokana na wanaofanya
ukatili huo kuelewa, na watendewa pia kuzidi kuamka, juhudi zaidi
zilitakiwa kujipenyeza zaidi dhidi ya imani za kimila ambazo bado
zinashikiliwa katika sehemu mbalimbali za nchi.
"Endeleeni
kutumia kalamu zenu na vifaa vyenu vyote kupiga vita vitendo vyote
vinavyotokana na manyanyaso ya kijinsia ambayo hasa hutokana na mfumo
dume," alisema wence akiwaomba wahabari kufanya hivyo kwa ajili ya
kuendeleza juhudi za kutokomeza kabisa suala la unyanyasaji wa kijinsia.
Wence
alisema jicho la waandishi wa habari linasaidia kuwaelimisha wananchi
juu ya mambo mbalimbali yanafanywa kinyume cha seria,kuwaomba wanahabari
kufanya habari za kichunguzi juu ya ukatili wa kijinsia pamoja na
unyanyasaji wake.
Pia
aliongeza kwa kusema kuwa kwa sasa TAMWA imekijita katika kufuatilia
habari juu ya ukatili wa kijinsia pamoja na mauwaji ya watu wenye
ulemavu na kulenga hasa habari za kichunguzi ambazo zitaleta mabadiliko
kwa jamii yetu.
Kwa
upande wa waandishi wa habari wa nyanda za juu kusini walioshiriki
warsha hiyo wamesema kuwa wanafanya kazi hiyo katika mazingira
magumu,hivyo kuwaomba TAMWA kuwasaidia chombo cha usafiri kila mkoa ili
waweze kuwafikia wananchi waliopo vijijini na kupata taarifa zao.
Lakini
wakawataka wanahabri wengine kufanya kazi kwa kufuta weledi wao kutokana
na elimu walioipata wakiwa darasa na kwenye mafunzo mbalimbali.