SPD waibuka na ushindi Hamburg
Shangwe zimehanikiza tangu Hamburg hadi makao makuu ya chama cha SPD mjini Berlin.Baada ya ushindi katika uchaguzi wa jiji la Hamburg di...
https://samchardtz.blogspot.com/2015/02/spd-waibuka-na-ushindi-hamburg.html
Shangwe zimehanikiza tangu Hamburg hadi makao makuu ya chama cha SPD
mjini Berlin.Baada ya ushindi katika uchaguzi wa jiji la Hamburg diwani
mkuu Olaf Scholz anapewa nafasi ya kuvaa taji la uongozi wa taifa
hatamu za uongozi ,hivi sasa Olaf Scholz na chama chake cha SPD wanahitaji mshirika serikalini.Walinzi wa mazingira,ambao Scholz anasema angependelea kushirikiana nao madarakani wameshasema majadiliano ya kuunda serikali ya muungano yatakuwa magumu.
Chama cha Christian Democratic cha kansela Angela Merkel kimepata pigo kubwa.Waliberali wa FDP wamefanikiwa kukiuka kiunzi cha asili mia tano sawa na chama kipya Chaguo Mbadala kwa Ujerumani AfD kilichojikingia asili mia sita nukta moja na kuwakilishwa kwa mara ya kwanza katika bunge la Hamburg.
Mwenyekiti wa kundi la wabunge wa chama cha SPD,Thomas Oppermann anayaangalia matokeo ya uchaguzi wa jana huko Hamburg kama ishara njema kwa chama chao.
Ahadi za uchaguzi zitatekelezwa
Olaz Scholz anakwenda Berlin hii leo kwa mazungumzo pamoja na mwenyekiti wa cha cha SPD Sigmar Gabriel.Kutokana na ushindi wake huo wa pili,diwani mkuu wa Hambourg amepata nguvu katika daraja ya shirikisho.Hakuna katika uongozi wa SPD anaeweza kushindana nae kwa kujikingia wingi wa kura.Na kutokana na makadirio haba ya maoni ya wananchi kwa chama cha SPD sauti zimeshaanza kupazwa kama Sigmar Gabriel akiwakiliashe kweli chama chao katika uchaguzi mkuu mwaka 2017.
FDP washusha pumzi
Kwa mujibu wa matokeo ya awali,SPD wamejikingia asili mia 45,7-wamepungukiwa na kura kidogo ikilinganishwa na uchaguzi wa mwaka 2011.CDU kimepoteza asili mia 6 na kusaliwa na asili mia 15.9-matokeo mabaya kabisa kuwahi kujipatia chama hicho jijini Hamburg.Walinzi wa mazingira wamejiimarisha na kujikingia asili mia 12.2.Chama cha FDP kimefanikiwa kwa mara ya kwanza tangu kilipopigwa kumbo katika daraja ya taifa,kusalia katika bunge la jimbo kwa kujikingia asili mia 7.4.Huku chama cha siasa kali za mrengo wa kushoto die Linke kikijijenga kwa asili mia 8.4.