Rais wa Ujerumani kuwasili Jumatatu
Joachim Gauck, Rais wa Ujerumani. Rais wa Ujerumani Joachim Gauck anawa...
https://samchardtz.blogspot.com/2015/02/rais-wa-ujerumani-kuwasili-jumatatu.html
Rais wa Ujerumani Joachim Gauck anawasili Jumatatu jioni kwa ziara ya siku tano.
Akiwa nchini Rais Gauck atakutana na
Rais Kikwete, wabunge na wawakilishi wa mashirika ya kijami. Msafara wa
Rais Gauck pia utajumuisha wafanya biashara wakubwa kutoka Ujerumani.
Tarehe 4 Rais Gauck ataelekea Zanzibar
ambako atakutana na Rais Shein na baadae kuelekea Arusha. Akiwa mjini
Arusha Joachim atatembelea mahakama ya Afrika ya Haki za binadamu, Makao
makuu ya Afrika Mashariki na kuhutubia Bunge la Afrika Mashariki.
Akiwa Arusha Joachim pia atakabidhi
Kituo cha Uendeshaji wa mapambano dhidi ya Ujangili kilichooko Seronera
kwenye mbuga ya Serengeti na kilichoanzishwa na Shirika la Kisayansi za
wanyama cha Ujerumani cha Deutsche Zoologische Gesellschaft.
Rais Gauck ataondoka nchini kurejea Ujerumani Februari 6, akipitia Uwanja wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA).
Mkuu wa Serikali ya Ujerumani ni
Chancelor, ingawa nchi hiyo pia ina Rais. Tofauti na nchi nyingine zenye
mfumo kama huo ambako cheo hicho kinakuwa cha heshima tu, Rais wa
Ujerumani ana madaraka kiasi fulani yakiwemo kuingia Mikataba ya
Kimataifa kwa niaba ya nchi yake.
