Rais Gauck ziarani Zanzibar
Rais wa Ujerumani Joachim Gauck amewasili Zanzibar kwa ziara ya muda mfupi. Gauck alipokewa kwenye bandari ya Zanzibar na Rais wa visiwa...
https://samchardtz.blogspot.com/2015/02/rais-gauck-ziarani-zanzibar.html
Rais wa Ujerumani Joachim Gauck amewasili Zanzibar kwa ziara ya muda
mfupi. Gauck alipokewa kwenye bandari ya Zanzibar na Rais wa visiwa
hivyo Dr Ali Mohammed Shein na umati mkubwa wa wananchi.
Ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya siku sita nchini Tanzania, Gauck huko
Zanzibar anahudhuria pia kongamano la viongozi wa dini. Baada ya hapo,
rais Gauck anaelekea mjini Arusha. Mohammed Abdul-Rahman amezungumza na
mwandishi wetu wa visiwani Zanzibar Salma Said kufahamu jinsi wananchi
wa visiwa hivyo wanavyoiangalia ziara hiyo.Kusikiliza mahojiano hayo, bonyeza alama ya spika za masikioni hapo chini.