Flatnews

Rais El-Sisi asema Misri itajibu mapigo

Rais Abdel Fattah el-Sisi wa Misri Rais wa Misri amesema nchi yake ina haki ya kujibu mashambulio kw...


Rais Abdel Fattah el-Sisi wa Misri
Rais wa Misri amesema nchi yake ina haki ya kujibu mashambulio kwa namna yoyote ile inayoona inafaa katika kulipiza kisasi cha mauaji ya kundi la Wakristo wa madhehebu ya Coptic yaliyofanywa
na kikundi cha wapiganaji wa jihad nchini Libya wenye uhusiano na kikundi cha Islamic State.
Rais Abdel Fattah al-Sisi ametoa kauli yake kupitia televisheni ya taifa baada ya video moja kuonyesha mateka wapatao kumi wa kundi la waumini wa madhehebu ya Coptic kukatwa vichwa.
Waumini ishirini na mmoja wa madhehebu ya Coptic nchini Misri walitekwa nchini Libya wiki kadhaa zilizopita. Maandishi yaliyowekwa katika video hiyo yanaonyesha walilengwa kwa sababu ya dini yao. Misri imetangaza wiki moja ya maombolezo ya kitaifa kufuatia vifo vya watu hao.
Mamlaka ya Kiislam inayoongoza nchini Misri,-- Al Azhar -- imeshutumu mauaji hayo na kuyaita ni ya "kinyama". Maelfu ya Wamisri wamekuwa wakivuka mpaka kwenda kutafuta kazi nchini Libya licha ya ushauri wa serikali yao ya Misri kuwakataza wasiende huko.

Related

NEWS 5017529797198465759

Post a Comment

emo-but-icon

item