PICHA:Waigizaji wa Siri ya Mtungi na mashabiki wao walivyosherekea siku ya wapendanao " VALENTINE DAY"
https://samchardtz.blogspot.com/2015/02/pichawaigizaji-wa-siri-ya-mtungi-na.html
Kila mtu anakumbuka kivyake VALENTINE yake ilivyoenda yani, mashabiki wa tamthilia ya ‘Siri ya Mtungi’ walipata nafasi ya kuenjoy na mastaa wanaoonekana kwenye tamthilia hiyo, Cheche pamoja na Cheusi.
Fans hao walipatikana kwenye shindano lililofanywa kwenye kurasa za Siri ya Mtungi kwenye Facebook, Instagram na Twitter, kazi ilikuwa rahisi tu, kuwashawishi wasanii hao kwa kutuma nyimbo, picha na video.
Walioshinda ni wawili, Wery Kuli na Nargis Swizzan.
Walienjoy pamoja chakula cha mchana katika mgahawa wa Karafuu, pamoja na kupiga picha za ukumbusho.
Picha: Cheche na Cheusi katika picha ya pamoja na mashabiki wao mara baada ya kupata chakula cha mchana.