Flatnews

Obama:Vita ni dhidi ya magaidi si Uislam

Rais Barack Obama wa Marekani  Rais Barack Obama ameliambia kongamano dhidi ya misimamo mikali ya kidini akisema kuwa kuwa wako kwenye v...


Rais Barack Obama wa Marekani 
Rais Barack Obama ameliambia kongamano dhidi ya misimamo mikali ya kidini akisema kuwa kuwa wako kwenye vita si na Waislamu bali na magaidi waliouchafua Uislamu.

Bwana Obama amesema ni sharti dunia ikabiliane na itikadi zilizopindishwa na makundi kama Islamic State yanayochochea vita na kuwapa vijana mafundisho yenye misimamo mikali ya imani ya kidini .
Ameyasema hayo katika mkutano wa siku tatu unaofanyika mjini Washington ambapo amesema dunia inatakiwa kukabiliana na makundi ya aina hiyo.
Rais Obama ameeleza kuwa manung'uniko waliyonayo vijana lazima yashughulikiwe ili kuondokana na hisia za makundi yenye misimamo mikali ya kiitikadi.
Wawakilishi kutoka zaidi ya nchi sitini wanahudhuria mkutano huo ambao umekuja kufuatia mashambulio ya makundi ya Kiislam katika nchi za Denmark, Ufaransa na Australia.

Related

NEWS 5951545027088914858

Post a Comment

emo-but-icon

item