Nisha Kuwapa Elimu ya Maisha Mashabiki
MWIGIZAJI wa filamu nchini, Salma Jabu ‘Nisha’, amesema anatarajia kuachia kazi yake mpya aliyoipa jina l...
https://samchardtz.blogspot.com/2015/02/nisha-kuwapa-elimu-ya-maisha-mashabiki.html
MWIGIZAJI wa filamu nchini, Salma Jabu ‘Nisha’, amesema anatarajia kuachia kazi yake mpya aliyoipa jina la ‘Shida’, ambayo itatoa mafunzo kwa mashabiki kukabiliana na hali yoyote ya maisha.
Akizungumzia filamu hiyo hapo jana, Nisha alisema filamu hiyo inatarajia kuingia sokoni mwishoni mwa mwezi huu, ambapo ameweza kumshirikisha nguli mwingine, Gabo.
Alisema mashabiki wategemee mambo mengi mazuri zaidi kutoka kwake, kwani mara nyingi amekuwa akifanya kazi kwa mpangilio ili kuhakikisha anatoa vitu vyenye ubora.