India:Uhuru wa Dini kuheshimiwa
Waandamanaji wakikemea vitendo vya mashambulizi dhidi ya Makanisa Waziri Mkuu wa India,Narendra Modi...
https://samchardtz.blogspot.com/2015/02/indiauhuru-wa-dini-kuheshimiwa.html
Waziri
Mkuu wa India,Narendra Modi ameahidi kulinda uhuru wa imani ya dini na
kusema kuwa Serikali yake haitaruhusu kundi lolote la kidini kuwa na
chuki dhidi ya jingine.
Akihutubia jamii ya kikristo mjini Delhi, ametoa wito kwa makundi yote ya kidini kuheshimiana.
Wito huo umekuja baada ya mfululizo wa matukio ya mashambulizi dhidi ya Makanisa, matukio yaliyosababisha ghadhabu miongoni mwa jamii ya Kikristo.