Hata mnyama anaona soni
Mackie Mdachi Kwa ufupi Mwanadamu ambaye anakosa kabisa ‘hali’ hiyo hapo juu, je, tunamfana...
https://samchardtz.blogspot.com/2015/02/hata-mnyama-anaona-soni.html
Mackie Mdachi
Kwa ufupi
Mwanadamu ambaye anakosa kabisa ‘hali’ hiyo hapo
juu, je, tunamfananisha na kitu gani. Au tumweke kwenye fungu gani? Na
mara nyingi watu wa aina hiyo tabia zao ni aidha za ucheshi, upole na
kuonyesha aina ya kujipendekeza kwa wanajamii yaani ni wanafiki au
wazandiki-haswa.
Soni inaelelzwa ni ‘aibu, haya’, yaani tabia au
hali ya mtu kuogopa maovu au aibu yake isijulikane na watu. Fedheha,
hali ya kusitasita kusema au kufanya jambo kwa sababu ya kumheshimu mtu
mwingine. Hali ya kutoweza kumwangalia au kuangalia mtu machoni.
Mwanadamu ambaye anakosa kabisa ‘hali’ hiyo hapo
juu, je, tunamfananisha na kitu gani. Au tumweke kwenye fungu gani? Na
mara nyingi watu wa aina hiyo tabia zao ni aidha za ucheshi, upole na
kuonyesha aina ya kujipendekeza kwa wanajamii yaani ni wanafiki au
wazandiki-haswa.
Ukutanapo ghafla na simba porini, wawindaji hata
wana vijiji wanathibitisha ya kuwa mnyama huyo huinamisha kichwa chake
chini au hugeuka upande mwingine kwa soni na kutokomea porini. Vivyo
hivyo hata paka umkutapo jikoni amefunua chungu na kula kitoweo, naye
ghafla hukuangalia kwa soni na kuondoka jikoni.
Yawaje wewe kiongozi wa umma ukakosa soni kabisa?
Sisiti kabisa kusema wahusika wote wa kashfa ya wizi wa kujitakia
wenyewe ya IPTL-Escrow wasionewe ‘haya’ wala kusamehewa kwani hiyo siyo
ajali; na wala zile lugha za ‘ajali ya kisiasa zisiwepo asilaani; ukiwa
‘umehomola’ kisicho stahiki yako, wewe ni mwizi tu.
Ya-Musa na Firauni
Hadithi ya Musa ni njema yenye upendo huruma,
kuwajali na kuwathamini wanajamii wenzake Wana-Israeli, wakiwa katika
dhiki, umaskini, utumwa na mateso nchini Misri; chini ya himaya ya Farao
almaarufu Firauni. Naye Firauni pasina ‘soni’ ya aina yoyote ile
aliwatesa Wana Israeli. Soma Biblia-Kitabu cha Kutoka 3-10.
Hadithi hii inafanana na juhudi zilizofanywa na
waasisi wa taifa letu, hayati Mwalimu Julius K. Nyerere-Musa na baadhi
ya wenzake; ghafla tunakutana na ma-Firauni ni aibu mno na inasononyesha
jamii yote ya Watanzania ambao kila uchwapo wanapigana na maisha duni
waliyonayo pamoja na utajiri mkubwa walionao wa maliasili kadhaa nchini;
ambazo zinaliwa na wachache mchana kweupee.
Si-hao tu waliochota mabilioni ya fedha ilhali
wakijua ni fedha za umma, kwani hazikudondoka kutoka mtini au mbinguni
kwa ajili yao; wapo pia wapiga debe wao wa waziwazi waliwatetea kwa
nguvu zote; nao kwa kivuli ati cha kukinusuru chama na Serikali. Ebo!
Nao pia hawana ‘soni’ wanapindisha sheria na ndimi zao.
Chama kinaweza kuwapo hiki na kile na kingine
tena, lakini wanajamii yaani Wananchi ni wale wale ambao wanaendelea
kuzongwa na uhaba wa dawa, madawati, vyumba vya madarasa, maabara,
kipato duni, kukosa soko thabiti la mazao yao, elimu isiyokidhi, walimu
kukosa mishahara kwa wakati, kutopandishwa vyeo wafanyakazi, uhaba wa
maji, umeme wa mashaka na vinginevyo hata maji yasiyo salama.
Kwa hali hiyo bado wapiga debe na hao wezi wa
fedha za umma Tegeta-Escrow wanajifanya hamnazo na kuona ni haki yao
kutoka kwa ‘mungu’ wao dhidi ya wanajamii wote wa Tanzania.