DRFA YATANGAZA TIMU 18 ZILIZOTINGA 18 BORA
Chama cha soka mkoa wa Dar es salaam DRFA,kimetangaza timu 18 zilizofanikiwa kutingia katika hatua ya 18 bora (raundi ya pili) ya m...
https://samchardtz.blogspot.com/2015/02/drfa-yatangaza-timu-18-zilizotinga-18.html
Chama
cha soka mkoa wa Dar es salaam DRFA,kimetangaza timu 18 zilizofanikiwa
kutingia katika hatua ya 18 bora (raundi ya pili) ya michuano ya ligi ya
mkoa wa Dar es salaam.
Timu
hizo ni kutoka katika kundi (A) ambazo ni Red Coast,Yanga
U20,Changanyikeni na Ukonga UTD,kundi (B) Simba U20,Stakishari,Zakhem na
Beira Hotspurs,kundi (C) FFU,Sifa UTD,Pan Africa na Sinza Stars,huku
kundi (D) likitoa timu za Shababi,New Kunduchi,Ugimbi na Azania Ngano.
Timu
mbili zilizopata nafasi ya kuongezwa kwenye hatua hiyo ya pili,ni Sifa
Politan FC pamoja na Tuamoyo FC,zinazokamilisha idadi ya timu 18.
Makatibu
wakuu wa timu zote 18,wanatakiwa kufika katika ofisi za DRFA zilizopo
kwenye jengo la Machinga Complex Ilala (Ghorofa ya 3),siku ya jumatano
04/02/2015,saa 8 mchana,kukutana na kamati ya mshindano kwaajili ya
kupata utaratibu.
Baada ya kikao hicho DRFA itapanga makundi na kutoa ratiba ya kuanza kwa patashika hiyo.