DR. JAKAYA KIKWETE: MBALI YA HAWA WALIOJITANGAZA WANA CCM WENYE SIFA YA KUGOMBEA URAIS WAKO WENGI, DIAMOND ATIKISA SONGEA
https://samchardtz.blogspot.com/2015/02/dr-jakaya-kikwete-mbali-ya-hawa.html
Kutoka
kushoto wengine ni Ndugu Abdulrahman Kinana Katibu Mkuu wa CCM, Waziri
Mkuu Mh. Mizengo Pinda na Makamu Mwenyekiti wa CCM Mzee Philip
Mangula(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-SONGEA)
Mwenyekiti
wa Chama cha Mapinduzi Rais Jakaya Kikwete akiongozana na Katibu Mkuu
wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana wakati alipowasili kwenye uwanja wa
ndege wa Songea mkoani Ruvuma.
Mwenyekiti
wa Chama cha Mapinduzi Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na Mkuu wa
wilaya ya Songea mjini Bw. Joseph Mkirikiti wakati alipowasili mkoani
humo kwa ajili ya kushiriki maadhimisho ya miaka 38 ya CCM kushoto ni
Mh. Said Mwambungu Mkuu wa mkoa wa Ruvuma.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Rais Jakaya Kikwete akitaniana na Mbunge wa jimbo la nyasa Mh. Kapteni John Komba.
Mwenyekiti
wa Chama cha Mapinduzi Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na wakuuu wa
vyombo vya ulinzi na usaliama wakati alipowasili kwenye uwanja wa ndege
Songea mkoani Ruvuma
Mwenyekiti
wa Chama cha Mapinduzi Rais Jakaya Kikwete akiangalia ngoma mbalimbali
zilizokuwa zikitumbuizwa na vikundi mbalimbali vilivyompokea leo kwenye
uwanja wa ndege wa Songea mkoani Ruvuma.
Waziri
Mkuu mstaafu Mh. Edward Lowassa akipokelewa na viongozi mbalimbali wa
mkoa wa Ruvuma kulia ni John Komba mbunge wa jimbo la Nyasa na kutoka
kushoto ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Singida ndugu Mgana Msindai na Mkuu
wa Wilaya ya Songea mjini Ndugu Joseph Mkirikiti.
Naibu
Katibu Mkuu wa CCM Bara na Naibu Waziri wa Fedha na Uchumi Mh Mwigulu
Nchemba akipokelewa na Nape nnauye Katibu wa Itikadi na Uenezi wakati
alipowasili kwenye uwanja wa Majimaji.
Star
Tv wanastahili kupongezwa kwa kazi waliyoifanya leo kwani kazi yao
ilikuwa imetulia na imepongezwa na watu wengi waliokuwa wakifuatilia
kwenye luninga huyu ni mmoja wa wapigapicha wa kituo hicho akifanya vitu
vyake.
Baadhi ya wazee waliofika kwenye maadhimisho hayo wakipelekwa eneo la kukaa.
Mzee
Philip Mangula Makamu Mwenyekiti wa CCM bara katikati, Mwenyekiti wa
Kamati ya Maandalizi Dr. Emmanuel Nchimbi na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu
Abdulrahman Kinana wakimsubiri Mwenyekiti wa chama hicho Dr. Jakaya
Kikwete kuwasili.
Mwenyekiti
wa Chama cha Mapinduzi Rais Jakaya Kikwete akiwasili kwenye uwanja wa
Majimaji huku akiwapungia mikono wana CCM na wananchi aliojitokeza
katika maadhimisho hayo yaliyofana.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa majimaji.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Rais Jakaya Kikwete akivishwa skafu na vijana wa chipikizi mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa Majimaji mjini Songea.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Rais Jakaya Kikwete akipokea heshima kwa kuimbiwa wimbo wa taifa na vijana wa chipukizi.
baadhi ya vijana wa chipukizi wakiimba wimbo wa taifa kwenye uwanja wa Majimaji katika maadhimisho hayo yaliyofana.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahmana Kinana kulia pamoja na wanakamati ya maandalizi wakiimba wimbo wa taifa.
Mwenyekiti
wa Chama cha Mapinduzi Rais Jakaya Kikwete akikagua gwaride la
chipukizi wakati alipowasili kwenye uwanja wa Majimaji mjini Songea
tayari kwa kuongoza maadhimisho ya miaka 38 ya CCM mkoani Ruvuma
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Rais Jakaya Kikwete akielekea jukwaani mara baada ya kukagua gwaride la chipukizi.
Mwenyekiti
wa Chama cha Mapinduzi Rais Dr. Jakaya Kikwete akipokea heshima wakati
gwaride la heshima la Chipukizi likipita na kutoa heshimza zake kwenye
jukwaa kuu.
Gwaride la heshima likipita mbele ya jukwaa kuuu na kutoa heshima.
Mpiganaji wa kituo cha Televisheni cha Star TV akifanya vitu vyake katika katika maadhimisho hayo.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi NDugu Nape Nnauye akizungumza jambo katika maadhimisho hayo
Umati wa watu waliojitokeza katika maadhimisho hayo.
Kapteni John Komba kulia na Abdul Misambano wa TOT wakiimba katika maadhimisho hayo.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimkaribisha Mwenyekiti wa CCM Dr. Jakaya Kikwete.
Mwenyekiti
wa Chama cha Mapinduzi Rais Jakaya Kikwete akiwahutubia wanCCM na
wananchi wa Songea mkoani Ruvuma wakati wa maadhimisho ya miaka 38 ya
CCM.
Mwanamuziki
Diamond Plutnamz akiimba katika uwanja wa Majimaji wakati wa
maadhimisho ya miaka38 ya CCM mjini Songea mkoani Ruvuma.
Mwanamuziki
Diamond Plutnamz akcheza katika uwanja wa Majimaji wakati wa
maadhimisho ya miaka38 ya CCM mjini Songea mkoani Ruvuma.
Mkuu
wa wilaya ya Songea mjini Mh. Joseph Mkirikiti akiwapooza wananchi wa
Songea kutulia ili Diamond Plutnamz kufanya vitu vyake jukwaani.