ALIEKUA MRS PLATNUMZ BI WEMA SEPETU AMTUSI SHEMEJI WA ZARI KWA KUVUJISHA PICHA AKILA UJANA NA MUME WA ZARI
Beautiful Onyinye, Wema Sepetu ‘Madam’. KIMENUKA! Beautiful Onyinye, Wema Sepetu ‘Madam’ amemporomoshea
https://samchardtz.blogspot.com/2015/02/aliekua-mrs-platnumz-bi-wema-sepetu.html
Beautiful Onyinye, Wema Sepetu ‘Madam’.
KIMENUKA!
Beautiful Onyinye, Wema Sepetu ‘Madam’ amemporomoshea matusi mazito
shemeji wa Zarina Hassan ‘Zari’, King Lauwrance akidai amemuudhi sana
kwa kitendo cha kuvujisha picha inayomuonesha akiponda raha nchini
Afrika Kusini ‘Sauz’ na mume wa Zari, Ivan Semwanga, Risasi Mchanganyiko
linakupa mchapo kamili.
Mwishoni
mwa wiki iliyopita, Wema na staa wa Bongo Fleva, Omari Nyembo ‘Ommy
Dimpoz’ walikwenda Sauz kurekodi video ya wimbo wa msanii huyo ambao
jina lake bado halijafahamika mara moja ndipo baadae picha ya Ivan, Wema
na King Lawrence ilipovuja na kuzua gumzo.
Kwa
mujibu wa chanzo chetu kilichokuwa Sauz, baada ya Wema na Ommy kutua
nchini humo na ‘project’ hiyo ya video, King Lawrance alidaiwa kuandaa
mpango kabambe wa kuhakikisha kwa namna yoyote wanaonana na Wema kisha
kupiga naye picha ambayo akiivujisha mtandaoni kila mtu ataamini
wamefanya malipizi kwa zilipendwa wa Wema, Nasibu Abdul ‘Diamond’ ambaye
amemnyakua Zari, mke wa Ivan.
“Ilikuwa
ni mpango wa malipizi, King na Ivan walikuwa wanaumia moyoni kumuona
Diamond anatoka na Zari wakati wao wana fedha kuliko Diamond hivyo
waliposikia mtoto wa kike (Wema) yupo Sauz wakasema watadili naye hadi
kieleweke, iwe ni kwa kufanikisha zoezi la kutoka naye kimapenzi au hata
kupiga picha ambazo zikisambaa mitandaoni, watu watajua kwamba
wamefanya malipizi,” kilisema chanzo chetu.
King Lauwrance (kushoto) akipozi na Ivan( aliyekuwa mume wa Zari).
KING AFANIKIWA KUIVUJISHA
Chanzo
hicho kilizidi kumwaga ubuyu kuwa, baada ya kufanya project, Ommy na
Wema usiku walikwenda katika moja ya klabu kula bata ndipo King na Ivan
walipozama na kufanikiwa kupata picha na Wema wakiwa katika kochi moja
kisha akaitupia katika mtandao wa Istagram.
“Wema
aliwachukulia kama washkaji, hakujua jamaa walikuwa na lao kichwani,
walipofanikiwa kupata picha tu, wakaitupia mtandaoni fasta na kufanya
Wema atukanwe na watu,” kilisema chanzo hicho
WEMA ACHARUKA
Baada ya
picha za Wema na Ivan kusambaa kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii,
mwandishi wetu alimtafuta Wema kwa njia ya simu ambapo alimcharukia King
kwa matusi mazito ambayo kimaadili hayandikiki gazetini hata mtandaoni.

Zarina Hassan ‘Zari’ akipozi.
“Yule
ni...(tusi) ameniboa kweli...(tusi) unajua vitu vingine vya kipuuzi
kabisa, wanatafuta kiki zisizokuwa za msingi wa...(tusi)” alisema
Wema.Wema alisisitiza kuwa hataki kumzungumzia sana King kwani anaamini
akifanya hivyo atamuongezea umaarufu ambao amekuwa akiutafuta muda
mrefu.
King
Lawrence amekuwa akimtusi Diamond mara kwa mara kwenye mitandao ya
kijamii huku akionesha jeuri ya fedha kwa kile kinachoonekana kuumia
kwake roho kwa kijana wa Tandale kumchukua shemeji yake Zari, aliyezaa
na Ivan watoto watatu.
CREDIT: GPPL