PICHA- BIBI ANAYEDHANIWA KUWA MCHAWI AKUTWA AKIWA UCHI HUKO MAGEUZI MJINI SHINYANGA
Hapa ni katika mtaa wa Mageuzi kata ya Ndembezi mjini Shinyanga pichani ni wakazi wa Ndembezi wakishuhudia tukio hilo la aina yak...
https://samchardtz.blogspot.com/2015/01/picha-bibi-anayedhaniwa-kuwa-mchawi.html
Hapa ni
katika mtaa wa Mageuzi kata ya Ndembezi mjini Shinyanga pichani ni
wakazi wa Ndembezi wakishuhudia tukio hilo la aina yake limevuta hisia
za wakazi wa kata ya Ndembezi huku wengine wakidai kuwa bibi huyo ni
mchawi kutokana na kiburi alichokuwa nacho huku akidiriki kupiga watu na
kwamba mikono yake inaonekana imekatwa panga na imekomaa sana ambapo
wataalamu wa mambo walisema huenda bibi huyo huwa anajigeuza Fisi na
kutembelea mikono-picha na Kadama Malunde-Shinyanga
Bibi(aliyeko
pichani) ambaye hajulikani jina wala anakotoka na ndiyo huyo amezua
kizaa zaa baada ya kukutwa nje ya nyumba ya mkazi wa mtaa huo aitwaye
Suzana Mwandu akiwa uchi wa mnyama hajitambui huku akitembea kwa kutumia
makalio yake.Baada ya kukutwa akiwa uchi wasamaria wema waliamua
kumvalisha nguo kusitiri mwili ingawa bibi huyo alijaribu kuzivua lakini
baadaye kutulia na kuanza kuzungumza maneno yasiyoeleweka -picha na
Kadama Malunde-Shinyanga
Mwonekano wa mikono ya bibi huyo iliyoonekana kama imekatwa kwa mapanga na imekomaa kwa nyuma-picha na Kadama Malunde
Malunde1
blog iliyofika eneo la tukio haraka iwezekanavyo kama kawaida yake
imeambiwa kuwa bibi huyo ambaye hakujulikana jina wala makazi yake awali
alikuwa haongei na aliposemeshwa ndipo akaanza kuongea kwa lugha ya
Kisukuma maneno yasiyoeleweka huku akisikika akisema wenzake wamemuacha
alikuwa anaenda kwenye sherehe-picha na Kadama Malunde-Shinyanga
Hatimaye bibi akaweza kusimama na kuanza kufanya vituko vya kila aina-picha na Kadama Malunde-Shinyanga
Bibi
akaamua kukaa na kuanza kutoa pesa alizokuwa amezifunga kiunoni kwa
kwenye mfuko wa rambo laini uliokuwa umefungwa kitaalam-picha na Kadama
Malunde-Shinyanga
Bibi akiangalia pesa zake-picha na Kadama Malunde-Shinyanga





