Naibu Waziri wa Mambo ya Nje amwakilisha Rais Kikwete kwenye Mkutano wa Wakuu wa Nchi wa NEPAD
Meza Kuu wakati wa Mkutano wa Wakuu wa Nchi wa NEPAD uliofanyika leo jijini Addis Ababa. Wakuu wa Nchi pamoja na mambo mengine wal...
https://samchardtz.blogspot.com/2015/01/naibu-waziri-wa-mambo-ya-nje.html
 |
| Meza
Kuu wakati wa Mkutano wa Wakuu wa Nchi wa NEPAD uliofanyika leo jijini
Addis Ababa. Wakuu wa Nchi pamoja na mambo mengine walisomewa taarifa ya
utekelezaji wa majukumu ya NEPAD kwa kipindi cha mwaka 2014. Kubwa
lilihusu uanzishwaji wa Mpango wa Kilimo unaozingatia mabadiliko ya
tabianchi ambao unawalenga wakulima wadogo zaidi ya milioni 25
watakaokuwa wanalima kwa kutumia teknolojia isiyokuwa na athari katika
tabianchi ifikapo mwaka 2025. |
 |
| Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini naye alishiriki mkutano huo |
 |
| Naibu
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Dkt. Mahadhi
Juma Maalim (Mb) alimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete katika Mkutano huo |
 |
|
Anayefurahia jambo ni Bibi Zulekha Tambwe, Afisa kutoka Wizara ya
Mambo ya Nje na nyuma yake ni Bw. Adam Issara, Katibu wa Naibu Waziri.
|