MOURINHO ANUNA NA KUWAGOMEA WAANDISHI WA HABARI......
+6 Jose Mourinho na Diego Costa wakizungumza wakati wa mechi dhidi ya Liverpool
https://samchardtz.blogspot.com/2015/01/mourinho-anuna-na-kuwagomea-waandishi.html
Jose Mourinho amenuna baada ya chama cha
soka England, FA kusema kinamtoza faini Diego Costa kwa kuonesha mchezo
usiokuwa wa kiungwana.
Mourinho ameichukia FA na anaamini
mfungaji wake anayeongoza kufumania nyavu ametolewa kama mbuzi wa kafara
kufuatia kumchezea vibaya beki wa Liverpool, Emre Can.
Kocha huyo wa Chelsea ambaye amewahi
kutozwa faini na FA alitakiwa kuwa na mkutano na waandishi wa habari
kesho ijumaa kuelekea mechi ngumu dhidi ya Manchester City jumamosi,
lakini ameufuta.
Diego Costa alionekana kumkanyaga mguu wa kulia Emre Can kwenye mechi ya nusu fainali ya Capital One dhidi ya Liverpool
Costa anaweza kufungiwa mechi tatu baada ya kutozwa faini na FA kutokana na kitendo hicho alichomfanyia Can.
Klabu ya Chelsea imefuta ratiba ya
mkutano na waandishi wa habari na hatawathubutu hata kumtuma kocha
msaidizi, Steve Holland kuzungumza na vyombo vya habari.
Imethibitishwa kuwa kikao cha nidhamu cha FA kitakachokaa kesho kitamuadhibu Costa.
Licha ya Costa kukataa kosa lake,
mshambuliaji huyo wa Chelsea anatarajia kufungiwa mechi tatu kuanzia ya
jumamosi dhidi ya Man City.