MAJANGAZI!!! MAGEREZA YA BRAZIL YAFURIKA
Wafungwa wa nchi ya Brazil. MAGEREZA NCHINI Brazil yamejaa wafungwa, hasa yale yenye watuhumiwa walikokutwa na kesi kubwa kubwa ziki...
https://samchardtz.blogspot.com/2015/01/majangazi-magereza-ya-brazil-yafurika.html
MAGEREZA NCHINI Brazil
yamejaa wafungwa, hasa yale yenye watuhumiwa walikokutwa na kesi kubwa
kubwa zikiwemo za kukutwa na biashara ya madawa ya kulevya.
Kutokana na wingi wa wafungwa hao, wamesababisha kutokea kwa vurugu za mara kwa mara zinazosababisha matumizi ya nguvu kubwa kutoka kwa vyombo vya usalama, wakiwemo polisi.
Kwa mujibu wa ripoti zilizotolewa, jumla ya wafungwa 75 waliuawa katika gereza la Pedrinhas Complex kuanzia mwaka 2013.
Katika mwaka huo, wafungwa watatu waliuawa kinyama kwa kuchijwa kufuatia vurugu kubwa zilizotogea gerezani hapo, zilizosababisha watu 60 kupoteza maisha.
Wafungwa wanafanya fujo hizo licha ya kuwapa kwa askari walio na vifaa vyote vya usalama kama bunduki nzito, mabomu na gesi.
Chanzo cha vurugu zinazotokea katika magereza mengi nchini Brazil, kinatajwa kuwa ni kitendo cha kuwachjanganya wafungwa kutoka makundi yaliyohamisiana kutokana na biashara ya dawa za kulevya.
Kwa mujibu wa ripoti zilizopo, Brazil ni nchi ya nne duniani iliyo na wafungwa wengi katika magereza yake, ikiwa na jumla ya watu 550,000, wakiwa nyuma ya Marekani,
Urusi na China.
Kutokana na matukio ya uhalifu ndani ya magereza, ikiwa ni pamoja na wafungwa wengi kutoroka, vifaa maalum vya kuangalia usalam vimefungwa (CCTV) huku pia kukiwa na askari wengi wa kulinda doria.