HIVI NDIVYO JUX ALIVYO WAJIBU WALIOHOJI KWANINI HAJAWAHI KUPOST PICHA YOYOTE AKIWA CHUO ANAKOSOMA NCHINI CHINA..AU HASOMI ?
Mastaa wengi wamekuwa wakiutumia mtandao wa Instagram kupost picha ambazo zinaonesha maisha yao na karibia kila wanachofany...
https://samchardtz.blogspot.com/2015/01/hivi-ndivyo-jux-alivyo-wajibu-waliohoji.html
Mastaa wengi wamekuwa wakiutumia mtandao
wa Instagram kupost picha ambazo zinaonesha maisha yao na karibia kila
wanachofanya, lakini kwa msanii wa R&B Juma
Jux kuna mstari ambao
ameuweka kati ya vitu anavyoshare kwenye mtandao huo na maisha yake
binafsi.
Inafahamika kuwa Jux anasoma nchini
China, lakini hajawahi kupost picha yoyote ikionesha yuko kwenye
mazingira ya chuo kama ambavyo labda hupost akiwa kwenye bata au akiwa
na washkaji zake au kwenye show.
Baada ya kuulizwa kama kuna mambo
mengine anayoyafanya huko tofauti na chuo, na kama kweli anasoma ni
kwanini hajawahi kushare na mashabiki wake picha zozote za mazingira ya
chuo, haya yalikuwa majibu yake.
“Nachoamini mimi hapa unajua mimi
katika maisha yangu, Instagram ni profile yangu mimi naamua nifanye nini
sifanyi kwasababu ya watu, pia najua mimi ni msanii kuna watu
wananiangalia kuna vitu flani siwezi kuvuka nikavifanya, “ Jux alisema.
“Darasani sio sehemu ya kupiga picha
umuoneshe mtu, kwanza darasani kwetu hairuhusiwi kupiga picha, haiwezi
kuwa mwalimu yupo anafundisha halafu unapiga nioneshe watu, no.
Nazingira yangu ya nje ya chuo ndio nafanya vile haya ni maisha yangu ya
nje ya chuo, lakini chuo nikienda naenda kusoma siendi kupiga picha,
kama mtu haniamini kwamba mimi nasoma nafanya vitu vingine sina power
zaidi ya kushawishi watu waniamini zaidi ya msemo wangu kwamba mimi kule
nasoma, siwezi kwenda darasani nipige picha niko na madaftari no,
lakini mimi nasoma niko kule kwasababu ya masomo.”