BUNGE laamrisha EWURA kufanya upya ukokotoaji na kupunguza bei ya mafuta ili kumnusuru mwananchi wa kawaida
Saturday, January 31, 2015
https://samchardtz.blogspot.com/2015/01/bunge-laamrisha-ewura-kufanya-upya.html
Saturday, January 31, 2015
Mamlaka
ya udhibiti wa huduma za nishati na maji EWURA imetakiwa kufanya upya
ukokotoaji na kupunguza bei ya mafuta ili mwananchi wa kawaida anufaike
na punguzo la bei ya bidhaa hiyo katika soko la Dunia badala ya
kuwanufaisha wafanyabiashara wakubwa wa bidhaa hiyo pekee sambamba na
kuangalia namna ya kuishirika sekta binafsi katika sekta ya gesi.
Agizo
hilo la Bunge kupitia kwa kamati ya kudumu ya nishati na madini
limetolewa bungeni mjini Dodoma na Mh .Juma Abdala Jjwayo wakati
akiwasilisha taarifa ya kamati hiyo bungeni ili kuwapa fursa wananchi
kunufaika na punguzo hilo badala ya kuwanufaisha wafanyabiashara wakubwa
pekee huku kamati ya kudumu ya bunge ya miundo mbinu Peter Serukamba
akisisitiza ulaazima wa usafiri wa reli kufufuliwa.
Mara
baada ya kuwasilishwa kwa taarifa hiyo baadhi ya wabunge waliopata
fursa ya kuchangia wametaka serikali kutilia msisitizo kwenye miundo
mbinu inayowagusa watanzania wote badala ya wale wenye kipato cha juu
pekee,pia kupunguzwa kwa bei ya mafuta na nishati pamoja na kuhakikisha
wafanyakazi wanaohudumia sekta ya reli wanalipwa stahiki zao kwa wakati.
Aidha
pia wabunge wengi akiwemo mbunge wa simanjiro Mh. Christopher Ole
Sendeka wamegusia suala la mradi wa usambazaji wa nishati ya umeme
vijijini yaani REA na kutaka serikali kuhakikisha inatenga fedha za
kutosha kuukamilisha mradi huo na kwamba suala la kupeleka na kusimika
nguzo pekee halitoshi.