UFARANSA YAICHAPA URENO NA C.RONALDO AKIWEMO
Mshambulizi Karimu Benzema alifunga bao la mapema na akatengeneza lingine kwa kiungo Paul Pogb...
https://samchardtz.blogspot.com/2014/10/ufaransa-yaichapa-ureno-na-cronaldo.html
Mshambulizi Karimu Benzema
alifunga bao la mapema na akatengeneza lingine kwa kiungo Paul Pogba
katika kipindi cha pili na kuisaidia Ufaransa kuibuka na ushindi wa
mabao 2-1 dhidi ya Ureno. RicaRrdo Quaresma alitokea benchi katika
kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Luis Nani katika dakika ya 68,
alifunga kwa mkwaju wa penalti dakika tisa baada ya kuingia uwanjamni .
Ufaransa ambao ndiyo wenyeji wa fainali zijazo za Ulaya waliifunga Ureno ambayo ilikuwa na mshambulizi wake mahiri na mchezaji bora wa dunia, Cristiano Ronaldo katika mchezo uliofanyika jijini Paris. Ronaldo alipiga mashuti manne katika mchezo huo lakini ni shuti moja tu ambalo lilikuwa na uhai. Timu zote zilicheza mchezo wa kufanana, Ufaransa walipiga mashuti 12 sawa na waliyopiga Ureno, lakini wageni walifanikiwa kupiga mashuti mawili tu ambayo yalimsumbua golikipa, Steven Mandanda.
Eliaguim Mangala, RAfaer Varane, Patrice Evra na Bacary SAgna walianza katika safu ya ulinzi na wanne hao hawakuwekwa majaribuni na kikosi kilichopoteza makali cha Ureno. Ronaldo alitoka uwanjani dakika ya 76 akimpisha Jose Mario alianza sambamba Danny na Nani katika safu ya mbele lakini watatu hao hawakuwa tishio kwa Ufaransa ambao walicheza jumla ya faulo 15 katika mchezo huo.