NEL AMPINGA MARINGA KESI YA PISTORIUS
https://samchardtz.blogspot.com/2014/10/nel-ampinga-maringa-kesi-ya-pistorius.html?m=0
Idara
ya kurekebisha tabia nchini Afrika Kusini inataka Oscar Pistorius apewe
kifungo cha nyumbani cha miaka mitatu kwa kumpiga risasi na kumuua
mpenziwe Reeva Steenkamp.
Bwana
Joel Maringa afisa anayehusika na masuala ya urekebishaji tabia
aliiambia mahakama mjini Pretoria kuwa hawamuadhibu tu Pistoruiis bali
pia wanataka kumbadili kitabia akisema kuwa anaweza kutoa huduma za
jamii kwa saa 16 kwa mwezi.
Awali
daktari wa Pistorius anayehusika na matatizo ya akili Lore Hartzenberg
aliiambia mahakama kuwa mwanariadha huyo mlemavu amevunjika moyo baada
ya kumuua mpenziwe.
Shahidi
wa tatu ambaye ni meneja wa shirika la Pistorius la Peet Van Zyl
aliiambia mahakama kuhusu orodha ya huduma zake zikiwemo za shirika la
kuwahudumia watoto la Umoja wa Mataifa kama balozi mwema. Kesi hiyo
inatarajiwa kuchukua muda wa siku tatu.
Kwa
upande wake mwendesha mashitaka Gerrie Nel ameelezea pendekezo hilo la
Bwana Maringa kuwa "linashtua na si sahihi"akisema zaidi kuwa ingekuwa
bora kusiwe na adhabu kabisa, huku akihoji kama Bwana Maringa alijua
ukubwa wa kosa la Pistorius.
Baba
wa Bi Steenkamp, Barry, alishika kichwa wakati Bwana Maringa
akizungumza, huku marafiki wa marehemu wakitikisa vichwa kwa mshangao wa
kile kilichoelezwa na Bwana Maringa.
Pistorius alipatikana na hatia ya kumuua Bi Steenkamp bila kukusudia mwezi uliopita -lakini aliondolewa mashitaka ya kuua.
Uamuzi huo ulishutumiwa na ndugu wa familia ya marehemu.
Pistorius
anakabiliwa na kifungo cha miaka 15 jela, japokuwa Jaji Thokozile
Masipa anaweza kuondoa kifungo hicho au kumtoza faini.
Amesema
mwanariadha huyo alifanya "uzembe" wakati alipompiga risasi mpenzi wake
kupitia mlango wa choo, akidhani ni mhalifu kutoka nje.