Marekani yawawekea ngumu madaktari wanaotoka Afrika Magharibi.
https://samchardtz.blogspot.com/2014/10/marekani-yawawekea-ngumu-madaktari.html
Utaratibu
ambao umewekwa na nchi hiyo ni ule unaowataka madaktari pamoja na watu
wengine wanaotokea ukanda wa Afrika Magharibi waliokuwa wakihudumia
waathirika wa Ebola kuwekwa karantini kwa siku 21 kabla ya
‘kujichanganya uraiani’ huko Marekani, ambapo New York na New Jersey
wameanza kuutekeleza utaratibu huo.
Zaidi
ya watu 8 waliougua Ebola Marekani, ambapo Nina Pham moja ya wauguzi
waliopata maambukizi wakati wakimhudumia Thomas Duncan aliyefariki kwa
ugonjwa huo, amepona maambukizi hayo na kupata nafasi ya kukutana na
rais wa Marekani, Obama ambaye walikumbatiana kitendo ambacho White
House imekielezea kuwa ni “namna ya kumsukuru Nina kwa huduma
anayojitolea”
Imeripotiwa
kuwa mtu wa kwanza kuripotiwa kuwa na maambukizi ya Ebola New York, Dk.
Spencer aliyepata maambukizi hayo akiwa Guinea hali yake inaendelea
kuimarika.