KUMBE RIYAMA NDO ALIONGEA UONGO HADI FRANK AKAKOSA DILI LA KUINGIZA UINGEREZA!!! SOMA ALICHOKISEMA FRANK HAPA.
https://samchardtz.blogspot.com/2014/10/kumbe-riyama-ndo-aliongea-uongo-hadi.html?m=0
MOHAMED
Mwikongi ‘Frank’ muongozaji na na mwigizaji nyota amefunguka kwa
kuelezea fitina na ubaya ambao amekuwa akifanyiwa Bongo Movie umemtisha
na anahisi sasa anatafutwa roho yake, kwani mara nyingi anapigwa vita
hadharani kutoka kwa wasanii wenzake ambao ujifanya ni marafiki.
Frank
anaelezea hayo baada ya mtayarishaji wa filamu ya Mateso Yangu
Ughaibuni kuweka bayana kuwa yeye hakumhitaji Issa Mussa katika filamu
yake bali aliyemchagua alikuwa ni Frank na baadae Riyama akamlaghai kwa
kumueleza kuwa Frank ni msumbufu bora ampe nafasi hiyo Cloud.
“Naomba
watu waniulizie dada yangu Riyama nimemkosea nini? Pamoja na kumsaidia
lakini ndio amekuwa mfitini wa kazi zangu, alishanifanyia unyama huo,
Shamsa Magunga katika kazi yake, leo tena karudia kwa Didas,”