Jibu alilolitoa Jay Z akitembea baada ya kumsikia mtu wa pembeni akiuliza Jay Z ni nani? (video)
https://samchardtz.blogspot.com/2014/10/jibu-alilolitoa-jay-z-akitembea-baada.html
Rapper
Jay Z na mke wake wapo Paris Ufaransa wiki hii ambapo wakati Jay akiwa
kwenye matembezi huku akiwa amembeba mtoto wake ilitokea mmoja wa
Watalii baada ya kumuona Jay akauliza ‘huyu ni nani? unajua jibu alilotoa mume huyu wa Beyonce?
Kabla
ya Jay Z kujibu, mlinzi wake aliekua ametangulia mbele hatua chache
huku Jay akifata kwa nyuma na timu yake alikua akizuia watu kupiga video
ambapo huyu mtalii alikua akipiga video, akawa anashangaa imekuaje
akatazwe kupiga video… swali lililoambatana na kuuliza huyu anaepita
nani? Jay Z kwa kiburi na yeye akamjibu kwa kuuliza ‘wewe ni nani?‘
Japo
inaonekana Jay Z alijibu kwa dharau, wataalamu wa mambo wanasema huenda
kweli mtalii huyu hakuwa anajua anaepita ni nani manake alikua kwenye
eneo la kitalii ambalo wengi wanaokuwepo hapo huchukua kumbukumbu
kupitia camera zao.