ITALIA YASHINDA 2-1 KUFUZU EURO
https://samchardtz.blogspot.com/2014/10/italia-yashinda-2-1-kufuzu-euro.html
YULE
mchezaji aliyeng'atwa meno na Luis Suarez kwenye Kombe la Dunia,
Giorgio Chiellini usiku wa jana amefunga mabao yote matatu peke yake,
Italia ikiilaza Azerbaijan 2-1 katika mchezo wa Kundi H kufuzu Euro The
Azzurri wakiendelea vizuri chini ya kocha
mpya, Antonio Conte.
Azerbaijan 'walipaki basi' wakicheza na
walinzi 10 na Italia ikapata tabu sana
kuupenya ukuta wao hadi Chiellini
alipotumia makos a ya kipa kuipa Azzurri bao la kuongoza dakika ya 44.
Chiellini
akajifunga kuisawazishia Azerbaijan dakika ya 76 katika harakati kuokoa
mpira wa kona- lakini bahati nzuri akasahihisha makosa yake kwa
kuifungia Italia bao la ushindi
dakika ya 82. katika mechi nyingine za Kundi H, Croatia imeifunga 1-0 Bulgaria bao pekee la Nikolay
Bodurov
la kujifunga dakika ya 36 na Norway imeifunga 3-0 Malta, mabao ya
Moeller Daehli dakika ya 22 na Joshua King dakika ya 26 na 49.