HABARI/PICHA:- MOTO WATEKETEZA SOKO URAMBO MKOANI TABORA
https://samchardtz.blogspot.com/2014/10/habaripicha-moto-wateketeza-soko-urambo.html?m=0
Moto
uliowaka zaidi ya masaa 9 umeteketeza meza zaidi ya 250 na maduka zaidi
ya 330 ya wafanyabiashana, huku wananchi wakihangaika kuuzima kwa
kutumia mchanga, katika soko kuu la mji mdogo wa Urambo mkoni Tabora
usiki wa kuamkia leo, katika kile, kilichohisiwa kuwa, unaweza kuwa
umesababishwa na mamarishe ndani ya soko.

Juhudi
za kumpata afisa biashara wa wilaya Bw. Hatibu Abdulahamani ili kujua
kiasi hasara walioipa wafanya bishara hao zinaendelea kutokana na
tathimini zinazoendelea kufanyika.